HIVI NI SAWA KUENDELEA KUKAA KWA KAKA YANGU BAADA YA KUOLEWA?

0

 


Nahisi kuchanganyikiwa, Kaka naolewa halafu naacha kila kitu. Mimi ni binti wa miaka 30, nina mchumba wangu ambaye Mungu akipenda mwezi wa sita tunafunga ndoa lakini Kaka mimi naishi na Kaka yangu, yeye kipato chake ni kikubwa na mimi ndiyo kila kitu kwa Kaka yangu.
Ananiamini kuliko hata mke wake na kila kitu nasimamia mimi. Baada ya mimi kupata mchumba Kaka yangu aliniambia kuwa siwezi kuondoka Dar kwani Biashara zake nyingi zitasimama, nilimuambia hamna shida kwakua mchumba wangu alikua anafanya akzi Dar, lakini wkenye haya mambo ya kuhamia Dodoma kahamishiwa.
Mchumba wangu ananiambia kuwa akishanioa ni lazima wote tukaishi Dododma, bado sijamuambia Kaka kwani nahisi kuwa atachanganyikiwa. Kaka hizi mali ni za Kaka yangu, simuamini kabisa mke wake wkaniana mambo ya Kishirikina na nahisi anamloga Kaka.
Naomba unisaidie, nifanye nini ili kumshawishi mchumba wangu mimi kubaki Dar kwa Kaka yangu au hata kwenye nyumba nyingine y Kaka ili kusimamia mali zetu. Mchumba wangu ni wale wanaume wakali na mara nyingi amekua akiniambia niachane na vitu vya Kaka yangu.
Lakini mimi ndiyo nimesoma kwetu, Kaka yangu ni Darasa la saba, mke wake ni mjanja, ana digrii, nahofia kama nikimuachia hivi vitu anaweza kutudhulumu na kuchukia kila kitu. Mama ananiambia kama mchumba wangu hataki nikae Dar ni bora tuahirishe harusi wanaume wapo wengi, kaka nampenda sana mchumba wangu lakini nahofia mali zetu zikiwa chini ya huyu mwanamke nisaidie hivi ni sawa mimi kuendelea kukaa kwa Kaka yangu baada ya ndoa?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top