NAKOSEA WAPI MKE MWENZANGU HATAKI TUWE MARAFIKI?

0

 Mimi ni Mama wa watoto wawili, nimeolewa ndoa yangu ina miaka 7 sasa. Mimi na mume wangu tulikua vizuri sana, lakini mwaka juzi alioa mke mwingine. Kabla ya kuoa aliniambia, hatukua na tatizo lolote lakini aliniambia ni kwasabababu ya Dini. Ingawa niliumia sana lakini nilimkubalia na nikaonahakuna shida.
Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, huyo mke mdogo nashindwa kumuelewa. Alipoolewa nilimpigia simu kumkaribisha lakinia linijibu vibaya, nikawa nampigia simu kumsalimia lakini hataki salamu zangu, anaishia kunisonya, nikimuambia mume wangu mbona mke mwenzangu hataki tuongee hataki urafikia anasema nimuache tu atazoea.
Kaka ni karibu mwaka wa tatu sasa nimeshaenda kwake mara moja ila hakunipoke vizuri, kwangu hajawahi kukanyaga na wala wanangu hataki kuwaona. Nashindwa kuelewa Kaka, niishije na mke mwenzangu, nikimueleza mume wangu ananiambia niachane naye, hivi Kaka watu mtaolewaje nyumba moja halafu muwe maadui?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top