NINGEKUA MIMI WEWE NINGEKUA NA SUBIRA KWANI NDOA HAIJI KWA HARAKA KIHIVYO!

0

 
Wanawake wengi, kila wanapofikisha miaka 25, wakitongozwa wanawaza ndoa. Najua, ndiyo, unakua ushamaliza chuo unatafuta kazi, au hukusoma sana hivyo uko mtaani muda mrefu, una maumivu ya nyuma umeshaumizwa kimtindo hivyo unataka mtu siriasi wa kukuoa.
(1) Mwanaume anakuja, anakupa stori za hapa na pale na kukuambia anataka kukuoa; Ukweli nikuwa, haijalishi kakuambia nini, asilimia 95 ya mambo anayokuambia mwanaume kabla ya kukupata kimapenzi ni uongo ili tu akupate.
(2) Ameshakuapata, hajakuacha, amekaa na wewe miezi miwili au mitatu unaanza kukumbushia kuhusu ahadi zake za nyuma kuwa atakuoa; Ukweli nikuwa, miezi miwili mpaka mitatu mwanaume bado hajaamua kama anakupenda au la, hajaamua kuwa wewe ni mtu sahihi au la.
Tena mwingine inawezekana hata bado hajaachana vizuri na X wake. Ukipiga kelele katika miezi hii ya mwanzo ni ngumu sana kupata mwanaume kwakua, aliachana na X wake kwasababu ya kelele kama zako za unanioa lini, wakaanza kufanyiana vituko kisha anakuja kwako, hata miezi mitatu bado unaanza kelele za X wake kutaka ndoa, anona ni walewale una kisirani zaidi yake anakuacha.
(3) Anakuambia ubebe mimba ili iwe rahisi kukuoa kwkaua unaongelea sana ndoa; Ukweli nikuwa hajajiandaa kuwa baba, hajajua hata kama anamuoa nani, anakuambia ubebe mimba kwakua anaona umri wake unaenda na hana mtoto, pili anajua ukishabeba mimba yake humuachi hivyo hata asipokuoa kwakua una mtoto wake utaendelea kuwa wake, kamwe mtoto hajwahai kurahidisha kujitambulisha.
(4) Kwakua hajakuoa kamaalivyoahidi mwanzo unafikiri alikua anakudanganya, unakasirika na kumuambia, nakupa miezi miwili kama hakuna ndoa basi sitkutaki; Ukweli nikua hata kama mwanaume angekua na nia kweli ya kukuoa ukishamuambia hivi anaona kama unataka kumpangia maisha hivyo uanakuacha kwani anakuona mbabe.
(5) Mwisho tongozwa na furahia mahusiano, kama ndoa inakuja ije, lakini sio kwkua alikuahidi ndoa wakati anakutongoza ukaanza kelele sasa ile ndoa lini, dada utaishia kubadilisha wanaume kama mashati na wote watakukimbia kwa kudai ndoa. Ingekua ni mimi ningefurahia mahusiano wakati nikisubiri ndoa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top