NJIAPANDA; NIMEMFUMANIA MWANAMKE WANGU ILA HATAKI KUNISAMEHE

0

 

Kaka Idd habari ya kazi kaka Nina jambo linaloumiza Sana moyo wangu naomba nikushirikishe nipate msaada maana ninaumia mno. Mimi ni Kijana wa miaka 33 nimetimiza juzi hapa Nilibahatika kupata mpenzi ambae nimedumu nae kwa miaka miwili pasipokuwa na shida Yoyote zaidi ya shida ndogo ndogo na tunasuluhishana.
Kilichonifanya nikuandikie huu ujumbe Kaka ni hivi Tarehe 16th March mpenzi wangu aliniandikia ujumbe na kuniuliza Niko wapi nikamwambia Niko nyumbani akasema anakuja Nikamwambia sawa karibu Baada ya dakika 20 akaniandikia tena ujumbe kwamba hataweza kuja tena ameamua Kukaa na ndugu zake Bar inaitwa.
Mimi nikasikitika kwasababu hapo nina kama miezi miwili sijaonana nae lakini sikuwa na jinsi nikaamua kukubaliana nae Baada ya muda kidogo nikamuomba tuongee hakujibu tena ujumbe wangu wala kusoma Hivyo nikaamua nitoke ninyooshe miguu sasa wakati nimetoka nikashangaa namuona mpenzi wangu yupo Bar ya nyingine sio ile aliyoniambia yuko na ndugu zake.
Nikajiuliza huyu ameniambia ameenda kule sas ahuku anafanya nini? Nikasema wacha nikae nione Walikuwa wamekaa wanaume wawili na wanawake wawili ambao ukiacha mpenzi wangu Mwanamke mmoja na mwanaume mmoja nawafahamu nikatulia pembeni kuwaangalia bila wao kuniona nikiwa nina mpigia simu hapokei anaiangalia nani amepiga halafu anafunika simu.
Kwakweli Kaka yangu niliumia sana kwasababu niliamini hakuna usalama. Kadri walivyokuwa wanaendelea kunywa pombe ndio matukio yalizidi kuniumiza sana Kwani mpenzi wangu alikuwa amesogeleana sana na yule kaka mwingine ambae simfahamu na wanashikana shikana niliumia na mpaka sasa ile picha haijatoka kichwani mwangu walikuwa wanakiss na kutomasana kwa mahaba sana.
Uvumilivu ukanishinda ikabidi nimfuate nikamwambia anachonifanyia sio vizuri. Aligeuka kuwa Mbogo kwa ukali na kunitukana sana niliumia sana kwasababu licha ya kumkuta na mwanaume mwingine alikuwa ananitukana nikaondoka na kumuacha pale nikarudi Mahali nilipokuwa nimekaa Waliendelea na mchezo wao licha ya mwanamke wangu kujua kua niko pale.
Mimi kinachoniuma sana sijawahi kumsaliti hata siku moja. Alinihakikishia kwa miaka yote hiyo niko mwenyewe kwenye moyo wake Kaka inaniuma mpaka sasa hivi baada ya kuona matendo yao machafu mbele yangu yanaendelea nikaondoka kurudi nyumbani sikujua kilichoendelea baada ya pale Kesho yake asubuhi nikampigia simu nikiwa na imani kwamba labda ni Pombe tu atakuwa amesahau na kukaa sawa ili tuongee badala yake alikuwa anakumbuka kila kitu.
Akaniambia alikuwa ananifanyia makusudi kwasababu simuamini alinitukana sana na kunidhalilisha ndugu yake mmoja akaomba kuonana nami nikasema afadhali niongee nae ili nipate auheni maneno aliyoniambia yule ndugu yake yaliniuma sana aliniambia Kaka najua unampenda sana dada yangu lakini kwa ulichokiona amekufanyia wewe hivyo je una uhakika gani kama hakuwahi kufanya kabla ya wewe kugundua yaliyotokea<
Akaniambia hiyo ni Tabia yake na hapo chagua mwenyewe kusuka au kunyoa Kaka nilikuwa naumia sana kwasababu ninampenda sana huyo binti niliamua kumuomba msamaha kwa yaliyotokea nikamuomba msamaha akasema amenisamehe Ila sasa amebadilika sana.
Nikitaka kuonana nae mpaka atake yeye Nikimtumia meseji anajibu anavyojisikia Kaka naumia nifanyaje na nina mpenda Sana huyu Dada Ninaumia mno kaka Bado namuomba msamaha anisamehe Ili arudi kama zamani Kwakuwa ninampenda sana na sijui ni kwa namna gani naweza kuishi bila yeye naomba ushauri wako.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top