SITAKI MWANAUME WAKUNIPOTEZEA MUDA NISHAUMIZWA SANA!

0

 Kama kila mwanaume anayekutongoza kitu cha kwanza ni kumuambia kuwa “Sitaki mwanaume wakunipotezea muda nishaumizwa sana!” basi jua kuna uwezekano mkubwa ukaishia kuumizwa, hakuna mwanaume ambaye anapenda mwanamke wa kauchwa achwa, mwanamke amabye ameumizwa sana. Kujitangazia kuwa wewe ni mtu wa kuumizwa ni kama dawa ya Mbu ikipulizwa chumbani hata kama chumba ni kizuri namna gani mtu lazima upige chafya na kutoka!
Kuachwa achwa ni matatizo, ni sawa na rafiki yako ambaye kila siku mkitaka kutoka yeye analalamika kuwa hana pesa, anatangaza matatizo yake. Hakuna mtu anataka kutoka naye out kwakua watu wanamjua kuwa ni mtu wa matatizo. Mwanaume akikuuliza kuhusu mahusiano yako ya zamani, acha kulalamika ukidhani kuwa atakuonea huruma ndiyo akupende sijui kama malaika, hapana, kwanza yeye mwenyewe katoka kuumiza huko!
Muambie nilikua na mtu tukashindwana nikaamua kuachana naye au nikaamua tutengane. Acha kulalamika kuwa wewe ndiyo uliachwa, acha kulalamika kuwa kuna mtu ulikua unampenda sana akakuacha na kakuumiza! Kwanza mwanaume akishajua kuwa kuna mwanaume mwingine ulikua unampenda mpaka kuchanganyikiwa anaamini huwezi kumpenda yeye sana hivyo anaona bore tu kukupotezea!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top