UKIONA MWANAMKE ANAKUFANYIA DHARAU ZA NAMNA HII BASI MUACHE AONDOKE!

0

  
Ukiona mwanamke wako anachepuka na kukuonyeshea waziwazi kuwa anawanaume wengine na kila ukiongea hajali au kila ukimfumania anaishia kukutukana na kukuambia msifuatiliane kama vipi basi muachane basi jua kuwa kashapima upepo na amejua kuwa huwezi kumuacha.
Inawezekana bado anakupenda au yuko na wewe kwakua kuna kitu anapata kwako, kwamba ingawa ana wanaume wengine wengi lakini wale wanaume kuna kitu ambacho hawampi, inaweza kuwa ni pesa, inaweza kuwa ni kumnyenyekea au labda kwakua mna watoto hawezi kukuacha hivyo wewe unakua ni mwanaume wake wa kunyanyasa na wale wengine ni wanaume wa kula nao maisha.
Kitu ambacho hukijui wewe ni kuwa, kama una mwanamke, anakufanyia vituko kila siku labda anakuendesha, anakutukana, ana wanaume wengine lakini hajali kuhusu wewe ni kuwa jinsi unavyoendelea kumuomba msamaha, kulia, kutafuta ndugu ili kusuluhisha ndiyo jinsi unazidi kumpa kiburi kuwa huwezi kumuacha.
Kama unataka abadilike kweli unapaswa ujifunze kuacha, anapokudhalilisha mbele za watu umuambie hapana, ondoka au kama unaishi kwake uondoke wewe na uendelee na maisha yako. Ukweli nikuwa, hicho kitu anachokipata kwako hata kama ni cha kijinga namna gani hawezi kupata kwa mwanaume mwingine yoyote yule na ipo siku atarudi. Hao wanaume wengine wanafurahia kuwa nayeye kwakua tabia zake zote mbaya anafanyia kwako siku akiwafanyia anayokufanyia hakuna rangia taacha ona!
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top