Ni sehemu ya maisha yetu kama wanadamu.Lazima ukubakliane na hali halisi kuwa kuna wakati utacheka ila kuna wakata yapo mambo yatakayo kuumiza
MWENZA WAKO ANAPO KUWA NA SIMANZI UNAFANAYAJE??
Una muacha aende akalale peke yake na simanzi moyoni??
una muacha alie mpaka atapo choka na kunyamaza??
Una amua kutoka maeneo aliyopo ili usisikie kelele zake ??
Au ndo utaendelea kumliza kwa kumpiga au matusi?
NDUGU YANGU KUWA SEHEMU YA TATIZO LAKE
Iwe analia sababu yako au sababu ya mambo mengine ni vyema ukaonesha kuumizwa na hali yake.Kama yupo jirani yako usione uvivu kumpa bega lako au kumlaza kifuani pake hata mapajani pako afu ukampatia nafasi alie mpaka pale atapo hisi kifua kupungua simanzi na hasira.
Kisha baada ya hapo hebu muulize taratibu tataizo na pendekeza cha kufanya.
Kama wewe ndo mkosaji basi omba msamaha hata wa kinafiki ili mradi uoneshe kuwa umekosea. Mwenza wako anayo haki ya kudeka kama mtoto kwako bila kujali umri wake wala elimu yake.
Kama anaishi mbali nawe labda mkoa au wilaya tofauti basi jitahidi kuwasiliana nae mara kwa mara iwe kwa text au kuongea kwa njia ya simu.Hiki ni kipindi anacho hitaji ukaribu wako kuliko kitu chochote kile.
Usiishi kwa mazoea,jifunze kubadilika kulingana na mazingira.Acha kuwa na roho ya JEUIR NA DHARAU ambapo mwenzako analia pembeni yako afu wewe upo bize na mambo yako.
Toka asubuhi ,mchana umegundua mwenzako hayupo sawa,usikubali alale usiku akiwa bado na simanzi.Tafuta namna ya kumpunguzia mawazo yake angalau usiku kwake uwe na ahueni..
Waweza toka nae nje mkazunguka, mkaenda pata kinywaji,au mkafanya matembezi ya kawaida.....
UNAJISIKIAJE
Mtu unalala nae kitanda kimoja lakini siku ya 1,2,3 hadi wiki kila mmoja hamsemeshi mwenzake?
wengine hufikia hatua ya kuwasiliana kwa sms tu na kuandkiana ujumbe mfupi na kuacha mezani.
Kwa nini uruhusu hali hii iitafune ndoa yako?? kila mmoja akisema awe juu ya mwenzake hamuwezi fika popote.
neno: POLE na SAMAHANI huwa hayabadilishi kitu kwa mtu mwenye tatizo lakini husaidia kurejesha tumaini na faraja.
Usichoke kuyatumia kila unapo pata nafasi wala huto pungukiwa na kitu..UTU NI BORA KULIKO KITU
Ila makosa na kero vikizid SAMAHANI itakosa nguvu