ASHIKILIWA POLISI KWA KUIBA MTOTO WA MIEZI MIWILI

0
#HABARI JESHI la Polisi Mkoa Geita linamshikilia mwanamke mmoja mkazi wa Kalebezo kata ya Nyamirembe wilayani Chato kwa tuhuma za kuiba mtoto mchanga mwenye umri wa miezi miwili.
:
Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halijafahamika anadaiwa kutenda tukio hilo Juni 27, mwaka huu.
:
Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo Hendry Mwaibambe, leo Juni 30 ambapo amemtaja mama wa mtoto huyo kuwa ni Eliada Juma (20) mkazi wa Nyabirere.
:
Mwaibambe amesimulia kuwa mama mzazi wa mtoto huyo alimuamini mtuhumiwa na kumkaribisha nyumbani kwake kama rafiki na alizoea na siku ya tukio alitoweka na mtoto akiwa amemfungia mgongoni kwa minajili ya kumbembeleza ili alale.

Credit-#NipasheMwangaWaJamii  #NipasheHabari

JE WEWE NI MPENZI WA SIMULIZ? BASI PATA KUSIKILIZA HAPA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top