♥ Yupo kwako akitafuta sex.. Tu .. Na kupunguzs stess zake.. Kwa hiyo utatumika kisha unawekwa kando
♥Kama ameweza kumsaliti mke wake.. Asilimia 100%haupo peke yako pia... Anawengine wengi anaowadanganya kama wewe
♥Ni kweli utaenda naye sehemu nzuri kutembea.. Lakini mwisho wa siku atarudi kwa mke na watoto wake... Na si kwako
♥Hata ukipata mimba hawezi kukuoa zaidi sana utaishiwa kufichwa na mwanao .. Watoto anawofahamu na kujivunia.. Wako watafichwa hadi mwisho
♥Angekuwa hampendi mke wake asingemuoa... Anampenda mwisho wa yote atarudi tu... Unajusumbua
♥Usitolee macho mali.. Ni zake na watoto wake
DADA ZANGU NI VIZURI KAMA MKIYAFAHAMU HAYA..!
👉 Mwili wako sio Maonesho, kila mwanaume auone.
👉 Mwili wako sio Mdoli kila mwanaume Auchezee.
👉 Mwili wako sio dampo, upokee kila uchafu wa mwanaume.
👉 Mwili wako sio Mali ya umma kila mwanaume akutumie.
👉 Mwili wako sio kiburudisho, kila mwanaume Ajiridhishe.
👉 Mwili wako sio pazia la Sebuleni, kila mwanaume Akufunue.
👉 Mwili wako sio karanga za kutembezwa mtaani kila mwanaume
Akuonje Utamu
🔹 Mwili wako ni wa Thamani sana. Mwili wako ndio utu wako.
🔹 Ebu Tunza Mwili wako nao Ukutunze. Uheshimu Mwili wako nao Utakuheshimisha.
🔹 Si kila mtu wa kuushika Mwili wako. Usitumie Mwili wako kama kitega uchumi, Usitumie Mwili wako kama dhamana ya kupata vile unavyohitaji.
🔹 Usitumie Mwili wako kama Njia ya kupata Mume Atakayekuoa. Kama Mungu amepanga Uolewe utaolewa tu
dada yangu hata bila ya kufunua Sketi yako. Muamini Mungu Yeye ndiye aliyeshikilia maisha yako.
🔹 Kuna mtu mmoja tu anayestahili kuugusa Mwili wako, kuuona Mwili wako, kuujua Uzuri wako.. Msubiri, Usiwe na Haraka, Mungu atamleta kwako. Endelea Kusubiri.
🔹 JITUNZE, JITHAMINI, JIKUBALI NA JIAMINI..!
SHARE NA WENGINE