Dalili 7 kuwa hujiamini na AFYA yako ya akili haiko sawa?

0

(1) Mume wako akichelewa kurudi, kabla ya kuuliza alikua wapi akili yako ishaanza kuhisi alikua na wanawake wengine, unapaniki, unapigia simu rafiki zake na kuanza kulia na kumtafuta.

(2) Mtu akikupigia simu na kukuambia nimemuona mume wako sehemu flani, kuna mwanamke amekaa naye. moja kwa moja kabla ya kuuliza huyo mwanamke ni nani? Kabla ya kumsikiliza, ushapaniki, ushajua ni mchepuko wake, unaanza kutuma meseji, kupiga simu mfululizo na kutishia hata kuondoka.

(3) Mwanaume wako asipojibu meseji zako hata kama yupo yuko online, moja kwa moja ushahisi anachart na wanawake wengine, unahisi anakudharau, unanuna, unaanza kulalamika, unapigia ndugu zake simu na wewe kulalamika kwa rafiki zako!

(4) Ukimpa ushauri mwanaume labda wa kufanya kitu flani, akaukataa basi unaanza kulalamika kuwa hakusikilizi, anasikiliza zaidi ndugu zake, anakudharau!

(5) Mwanaume wako akiwa karibu na ndugu zake, akisaidia rafiki zake hata kwenye mambo ya maana unahisi hakujali wewe, anakudharau na haoni umuhimu wako.

(6) Kama umesoma hii post badala ya kujifunza kuhusu mapunguifu yako na kujirakebisha umeanza kusema “Anatetea wanaume wenzake” bila kujua kuwa mwishoni ningeandika kuwa, kama mwanaume una tabia hizi basi jua kuwa nawe hujiamini unahitaji kubadilika.

(7) Hauko peke yako, hizi ni tabia za karibu kila mtu, kuna nyingine hata mimi ninazo hivyo taratibu kwa afya ya akili yako, jifunze kuanza kuacha tabia hizi kwani zinavunja mahusino mengi, zinaleta msongo wa mawazo na zinakufanya uhisi kuwa kila wakati unaonewa!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top