HATUA 5 ZA KUWA MUME MUUNGWANA MBELE YA MKE WAKO

0*USIMDANGANYE KUWA UTAMUOA KAMA HUNA UHAKIKA WA KUWA NAYE*
Acha kuchezea hisia za wanawake. Unaweza ukawa unalifurahia jambo hilo, lakini ni jambo ambalo mwishowe litamuumiza yeye. Unapaswa kuwa mwanaume wa kweli na umueleze ukweli. Mueleze hisia zako kwa ukweli na achana na uongo, kwani uongo sio sifa ya wanaume waungwana na wastaarabu.

*HESHIMU MAMBO YAKE BINAFSI*
Naam, bila shaka mahaba ni matamu, wewe na yeye ni mwili mmoja na kadhalika na kadhalika. Lakini mambo binafsi yanapaswa kuheshimiwa kwa kila upande. Epuka kupekua katika orodha ya waliompigia simu, usimuulize kila dogo na kubwa na yale aliyoyafanya na marafiki zake, mpe fursa ya kuwa yeye.

*MSIKILIZE ANAPOZUNGUMZA*
Rafiki yako anapozungumza huwa unamsikiliza kwa utulivu bila kumkasirikia. Kwa nini mkeo anapohitaji mtu wa kumsikiliza na kumsaidia kutatua matatizo yake hutaki kumsikiliza? Hakika kumpuuza na kutomsikiliza ni jambo baya sana.

*MPE AMANI NA UTULIVU*
Mfanye ahisi utulivu kupitia maneno yako. Unatakiwa kuwa naye katika nyakati ngumu na uwe mtu wa kwanza ambaye atamkimbilia wakati wa matatizo. Hilo litakuwa jambo kubwa sana kwake kuliko unavyofikiria.

*MHAMASISHE KATIKA NDOTO ZAKE*
Iwapo ana ndoto yoyote ile, basi unatakiwa kuwa mtu wa kwanza kumuunga mkono na kumpa hamasa. Yawezakana mkeo huyo ana vipawa vingi sana, usiwe mtu wa kwanza kumuangusha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top