HII NDIO SUMU YA NDOA TAFADHALI TAFUTA DAWA YAKE!

0
Kuna watu wengi wanawalaumu sana wenza wao kwa makosa yao wenyewe,kama wewe ni mwanamke na mume wako humfanyii vitu vifuatavyo na hujawahi kufanya naomba ujilaumu mwenyewe kwa kutosimama kwa ndoa yako.

1. Humfulii anafuliwa na housegirl na wewe upo hata kama unakazi kiasi gani ila jua mumeo n jukumu lako.

2. Mume wako hajui ladha ya chakula chako,'na hata kama anajua unajipikia pikia tu,jua baada ya tendo la ndoa mwanaume anakamatwa na msosi mzuri.

3. Unakiburi,jazba zisizo na maana.
Mume wako kachelewa bahati mbaya kurudi nyumban unanuna bila kuuliza alikuwa wapi au kapatwa na nini jua mchawi wa ndoa yako n wewe mwenyewe.

4. Hujawahi kumsafisha mumeo.
Hujui mume wako mara ya mwisho kumnyoa zivu ni lini,hujawahi mkata kucha,hujawahi kujua anatumia pafyumu ya aina gani,Dada yangu usimlaumu mtu kwa kusaidiwa majukumu
🌹🌹

5. Kikubwa zaidi kitu cha kwanza anachokula mwanaume asubuhi kabla hajaenda kazini hata kama ni chai nusu kikombe kina ipa baraka ndoa yenu,usiruhusu mume wako kuondoka bila kuingiza tumboni chochote kilichoandaliwa na wewe na sio housegirl.na kama una uwezo hakikisha amekunywa chai iliyopikwa na wewe kabla hajaenda kazini.

6. Hujawahi tenga muda kwa ajili ya kukaa na mume wako pekee yenu mkajadili mambo mbali mbali yanayohusu ndoa yenu,Dada yangu ubize upo ila tafuta hata siku moja kwa mwezi mkae sehemu tulivu mjadili mambo mbali mbali yanayohusu ndoa yenu.

Mwisho nasemea hivi Mwisho: Yaani neno mwisho munalielewa lakini? Yaani MWISHO: 

Najua kuna watakaosema muda huo hawana,au kazi hio wanawaachia michepuko au wanaume hawana shukrani lakini Dada yangu,Mama yangu ulipokuwa kwenye ndoa jua ndoa ni yako na wa kuijenga ni wewe sasa uamuzi ni wako.

Simlazimishi mtu kubeba nilichokiandika ila naamini kwa wale ambao wamenielewa watabeba kwa umakini Na watafanyia kazi 🙏🙏


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top