Hivi ndivyo unavyompoteza MWANAUME anayekupenda kwa kudhani hakupendi

0

Una mpenzi wako mnakaa mbali au hata sehemu moja lakini hamuonani kila siku, anakupigia simu mara kwamara na wewe unajisahau, unawaza kama ananipigia kuna haja gani ya kumpigia. Anakaa kimya kidogo unampigia, sasa unajitahidi kuchangamka na kuombea mambo ya kimahaba lakini yeye anakazania kwanini hunipigii, mnatumia nususaa kujadili kwanini humoigii simu au kujibu meseji zake.

Unatafuta kauongo kazuri labda unasema kuwa ulikua bize na kazi, mnatumia nusu saa nyingine kuzungumzia namna ambavyo unajali kazi yako kuliko unavyomjali yeye, anakukumbushia mambo mpaka ya miaka ishirini hata kabla hajakujua mpaka unashangaa huyu hasahau. Baada ya kupoteza lisaa lizima unataka kukata simu maana una kitu cha maana, sasa hata hamkati tena.

Mnatumia nusu saa nyingine kujadili kwanini humpi kipaumbele, hupendi kuongea naye huna kitu cha maana aunamkwepa tu, unamkatia simu au anajadili hao wengine huko ndiyo wamaana zaidi. Unaamua kunyamaza kumsikiliza lakini kuna sauti ya rafiki inasikika, anaanza kulalamika nusu saa kuwa uko na marafiki badala ya kuongea naye unapoteza muda nao.

Masaa mawili mtu mnaongea au hata nususaa mnaongea mnalumbana, nalaalamika hata kumuuliza kuwa kava nini hata mchangamshane mpige umbea wa kina Mange Kimambi hamna, analalamika tu! Dada yangu kama wewe ndiyo mpenzi wangu uko hivi hata mimi nisingekupigia simu, nani anataka ujinga wa namna hiyo? Yaani nina stress zangu badala tuongee ili niziondoe naongeza stress nyingine.

Hapa kama sikupendi sana nakupotezea mazima na kukublock na kublok kabisa, tukikutana nitaomba msamaha wa jumla unisamehe usinisamehe utajua mwenyewe. Lakini kama nakupenda, tena sio kupenda tu kama nakupenda sana kile cha kwenye TV, basi nitakua nikikupigia kila mwisho wa wiki ili ukilalamika unalalamika kwa pamoja na naomba msamaha wa jumla. Nishamaliza ila najua kuna na wanaume wengi tu wana tabia kama hizi! Najua wanasoma niwamabie tu kua “Mnawaboa wapenzi wenu!”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top