HIVI NDIVYO WANAWAKE WANAVYOTAPELIWA NA KUFANYWA SINGLE MOTHER

1

(1) Una kazi nzuri, una kipato chako tu kizuri lakini uko single na ni mpweke. Huna mtu au kila mwanaume unayekutana naye ni wale wanaonekana kuwa ni matapeli, wanaonekana kuwa hawataki kuoa. Lakini sasa hivi una miaka kuanzia 27, au una chini ya hapo ila kila siku unalalamika kuwa unataka mtu siriasi na unachagua mwanaume moaji.

(2) Anakuja kijana, anaweza kuwa mtu mzima kidogo, miaka yake ni kuanzia 30-45, mara chache sana wanakua chini ya hapo, hajaoa, au anakuambia kuwa aliwahi kuwa na mwanamke wana mtoto lakini waliachana. Anakuambia kuwa sasa hivi anataka mtu wakutulia naye,  ashazunguka sana na kuhangaika na wanawake hivyo anataka mtu wa kutengeneza familia.

(3) Mnakua marafiki  hazungumzii sana kuhusu  kufanya tendo la ndoa yeye anazungumzia ndoa zaidi, tena hata kama umemuambia mpaka ndoa ndiyo mtafanya mapenzi basi hana shida anakubali Kaka wa watu, anajalii na kila kitu anachoongea ni kama alikua kichwani kwako, yaani anaongea kile kitu unachotaka kusikia.

(4) Hapa anakupa mipango yake, yaani namna anavyotaka familia yake iwe, anakuambia mipango yake ya maendeleo na mambo kibao, inawezekana unajua anapofanya kazi lakini mara nyingi wanakua wafanyabiashara au anakuambia anafanya kazi sehemu flani ila hajawahi kukupeleka, wachache wanakupeleka. Lakini nasisitizi mipango yake ni mingi na anakushirikisha na kukuomba ushauri kwenye mambo yake ya maana.

(5) Anaweza kujitambulisha kwenu kwanza kama una kasi, lakini wakati mwingine hata kabla hajajitambulisha ataanza kukuomba vipesa. Utasikia “Pesa yangu imeishia kwenye ujenzi, unaweza kunisaidia kiasi flani… unajua wewe nakuona kama mke kunakitu nataka kufanya niongezeee kiasi flani… kuna tatizo flani limetokea sehemu flani labda kazini…”

(6) Haishii hapo, mara unaona anakupa michongo ya kibiashara anakuambia mambo yake yamekwama anahitaji milioni kadhaa, ukiangalia pesa anayotaja unakua nayo yaani ni kama alijua kuwa unayo. Au inawezekana huna ila anavyokuambia ni kama ukope na anjua kuwa unaweza kukopa kazini au sehemu…

(7) Hapo anakua spidi sana, anataka na mtoto atakua makini sana na kalenda yako na atahakikisha kuwa unabeba mimba. Ambao mshaliwa tayari kunai le mimba ambayo ulibeba ukadhani kuwa ilikua ni bahari mbaya, hapana mwenzo alipanga kwa watu kama hawa hakuna bahati mbaya kabisa.

(8) Umebeba mimba anakua karibu sana na wewe, sasa hivi anaweza kumuambia muishi pamoja, au inawezekana ashahamia kwako, lakini cha ajabu nikuw ayeye hahudumii kwa chochote, yaani akitoa ni kidogo sanaila kila kitu unatoa wewe. Inawezekana unamuamini zaidi kwakua ashajitambulisha kwenu hivyo unamuona wamaana sana, lakini hata kama bado, wewe kakutambulisha hata kama si kwa kukupeleka basi unaongea sana na ndugu zake mpaka unemuona mke.

(9) Kama una biashara atataka kuisimamia yeye, lakini kama huna biahsraa atataka mfungue, atakuambia chukua mkiopo, atakuambia mambo mengi, kwa stori zake yaani unajiona kesho ushafanikiwa, ni kichwa haswa ila yeye hatoi pesa na mkinunua kitu anaandika majina yake, hata kama wewe umechangia zaidi utasikia “Inamaana huniamini… Inamaana unaona kuwa nawez akukutapeli kitu kidogo kama hiki…”

(10) Umeshatoa pesa milioni kadhaa kakutapeli... kuna mimba ina jina lake na bado hajakuoa ndiyo unasikia kuwa ana mwanamke mwingine, mwanamke aliyekuambia alizaa naye tu ni mke wake au naye alitapeliwa kama wewe! Kama hukutoa pesa anakuacha na mtoto na hahudumii anahamia kwa mwanamke mwingine, lakini kwakua nawe ni mpweke unaendelea kuumia na kudhani kuwa atarudi.

Dada yangu hauko peke yako, kama ulishatapeliwa pole, lakini kama bado na unaona hizi dalili basi ukitaka kumpima kama anakupenda kweli. Fanya mambo yako kivyako usimshirikishe, acha kumpa pesa, anza kuomba wewe pesa kama mwanamke na usishobokee sana kutambulishana. Haita pita mwezi atakukimbia kwenda kutafuta mhanga mwingine!

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top