Changamoto za ndoa zisipopata tiba sahihi zinatesa kuliko kitu chochote katika uso wa dunia hii....
Ndoa ina nguvu na maumivu makali kuliko maumivu ya kitu chochote unachokijua chenye kusababisha Uchungu.
Ndoa ni eneo ambalo linaweza kukufanya kukata tamaa ya maisha, kukosa furaha, kujiona huna thamani, kupunguza furaha n.k
Ufanye nini unapokosewa /kutendwa na mpenzi unayempenda?
01 .Tumia muda wako kumtafakari Mungu kwa ajiri ya hilo kabla hujaenda kuomba ushauri n.k kwa kuomba na kumwombea Mwenza wako.
02. Tumia siraha kuu ya Ushindi wa kila changamoto ambayo ni Upendo, Upendo huongeza wingi wa furaha na amani kwa Mwanadamu ila chuki haijengi bali chuki hubomoa na upendo hustahimili na kumwezesha mtu kuweza mahali asipoweza, kitendo cha wewe Kumchukia mwenza wako kisa kakukwanza/kukukosea siyo tiba bali ni frusa ya kufungua mlango ili adui apate nasafisi ya kukushitakia
# 1kornt 13:4-7
"4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
Ni kweli amekuudhi na kukuumiza sana kwa hilo alilokutendea, lakini kuna wakati alikufaa sana na ulimshukuru. Usifute mema yake kwa huo ubaya mmoja aliokutendea bali waombee, mpende ili upendo wako kwake uwe tiba ya kumrejesha katika uzuri wa kwanza.
Barikiwa sana. Usisahau kutembelea page ya Facebook.com/idawamedia