ASEMA HAWAKO SAWA NA MKEWE ANATAKA KUNIOA! NASHINDWA KUMKATAA

0Habari Kaka sijui umri wako lakini naona kama kila mtu anakuita Kaka. Mimi ni mama wa miaka 45, sijaolewa ila nina watoto watatu, nimekua na mahusiano na mume wa mtu kwa miaka 10 sasa, yeye ndiyo nimezaa naye hawa watoto, ana miaka 47 kanizidi miaka miwili. Wakati nakutana naye aliniambia kuwa atamuacha mke wake, aliniambia kuwa yeye na mke wake wanagomana kila siku kwani mke wake hana akili ya maisha, ni mtu wa kutumia tu na hajuin namna ya kumuacha.

Tulianzisha mahusiano na yalikua ya wazi tu, mpaka sasa tuna watoto watatu mwanzo mke wake alikua akiongea ila lifikia hatua alikubaliana na ukweli kuwa mimi ndiyo napendwa na kukubali kuwa kuna mke mwenza. Tumeishi kwa amani, kila kitu Napata na kusema kweli pamoja na kuwa na mke wa ndoa ya kanisanani lakini alikua akitumia muda mwingi kwangu, mimi nafanya Biashara na bishara zetu tunafanya pamoja, nampa mawazo, tumefanya mambo mengi sana kama mke na mume.

Tatizo nikuwa kila nikimuambia tufunge ndoa ya serikali ananiambia kuwa nisubiri amuache mke wake kwanza. Nimekua nikibembelezea ndoa mpaka nikaona haina haja kwani kama naishi vizuri, nakula vizuri na tuna amani kwanini nihangaike. Sababu ya kuja kwako nikuwa, hivi karibuni niliona mchumba wangu kababadilika, haji tena kwangu, simu zake kaweka password, yaani kila kitu kikawa tofauti. Nilihisi labda karudiana na mke wake wapo vizuri, lakini nilichunguza na kugundua kuwa ishu si mke wake.

Kuna kadade kengine ten aka mwanafunzi kachuo katoto kadogo kana miaka 22 ndiyo kanamchanganya. Amempangishia nyumba masaki, nyumba nzima, amemnunulia gari Harrier milioni 28 na anampa kila kitu, anatumia muda mwingi kwa huyo mtoto mdogo na binti ana mdomo balaa. Niliamua kumtafuta huyo binti na kumuambia aachane na mume wangu kwani hajui tulipotoka, lakini kilichoniuma nikuwa mwanaume amemuambia kila kitu yule binti, amemuambia mimi si mke wake ni hawara tu, kabinti kamenitukana, amemuambia mpaka mambo yetu ya ndani.

Yaani kaa alivyokua ananiambia mimi mapungufu ya mke wake ndiyo anamuambia na yeye, amenitukana matusi ambayo siwezi kuandika hapa. Mimi nilisikiliza nikasema hapana, siwezi kutukanwa na kabiti kadogo kama haka, kwa bahati nzuri ni kama nilirekodi, lengo langu lilikua ni mwanaume akikataa basi nimsikilize. Lakini kutokana na kurekodi niliona kwanini ananitukana hivi, nikaenda polisi, binti akatafutwa na kukamatwa. Alikaa ndani siku mbili, mwanaume akaja akaniomba msamaha akasema alikosea atachukua kila kitu alichompa yule binti, alimkana binti mbele yangu na kumuambia kabisa kuwa mimi ni kama mke wake ana nanipenda.

Ili kuepusha mambo mengi na kwakua mume wangu ni mtu anaheshimika najua kuwa ile kesi ingemuathiri nayeye basi nilikubali kufuta kesi na kufuta zile clips. Ila kaka baada ya kufanya hivyo kwanza mwanaume alinipiga mpaka nikazimia, baada ya kuzindika aliniambia hanitaki, mimi ni nani kumchunga, mke wake hampangii maisha mimi Malaya ndiyo nimopangie. Alikasirika sana kwa mwanamke wake kuwekwa mahabusu, ameniambia kuwa hanitaki na nisimujue. Kaka kuna vitu vingi tumechuma na huyu mwanaume, kwanza tuna duka kubwa la vifaa vya ujenzi, tulianzisha pamoja lakini tulitumia TIN namba yake.

Tuna nyumba mbili moja ina majina yake na moja ina jina langu, tulifanya hivyo makusudi kwakua hatukua na ndoa, lakini tatizo nikuwa, nyumba zote tulichukulia mkopo. Wakati tunaanza ilikua hivi, mkopo wa kwanza yeye alichukua kwa kupitia nyumba yake ambayo alijenga mwenyewe, akaweka kwenye Biashara na mimi wakati huo nilikua na kazi, nikachukua mkopo ofisini kazini tukachanga ndiyo tukafungua hilo duka. Lakini akaniambia kuwa, kwakua yeye tayari ana nyumba ambayo anaishi na mke wake, ana ana nyumba nyingine ambaye alijenga tukiwa pamoja ni muhimu na mimi nikawa na nyumba.

Wakati huo nilikua na ujauzito wa mtoto wetu wa pili, nilikua na kiwanja changu kikubwa tu ambacho nilinunua kabla ya kukutana naye, tukaweka malengo pesa ya Biashara ndiyo tujengee. Kweli tulijengea mpaka nyumba ikakamilika, kubwa tu. Baada ya nyumba kukamilika maisha yaliendelea na Biashara iliendelea kuwa kubwa, tukanunua magari mawili Canter ya mizigo, yote yana majina yake, sikuona shida kwani kila kitu tulikua tunashirikiana. lakini mwaka huu aliniambia nichukue mkopo tufungue duka jingine ambalo lina jina langu, aliniambia kuwa sasa hivi duka lina jina lake, mfano likitokea la kutokea mimi naweza nsiipate kitu.

Alinishawishi nichukue mkopo kupitia nyumba yangu, Biashara yetu ndiyo italipa, akaniambia kuwa nifungue biahsara nyingine kwa TIN namba yangu, niliona ni wazo zuri kumbe alikua amenitapeli kwani pesa hizo ndiyo alitumia kumhonga mwanamke wake kumnunulia gari na kila kitu. Biashara inayumba na pesa zote za mauzo anachukua yeye, sioni hata shilingi kumi, ninafaanya kazi ndiyo lakini mshahara wangu una mikopo mingi naomba unisaidie nifanye nini ili angalau anisikilize, nikiongea na mke wake ndiyo hata hajali anasema ashazoea, sasa hii hali mpaka lini Kaka, nimekwama naomba unisaidie nifanye nini?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top