Mithali 16:1
"Maandalio ya MOYO ni ya mwanadamu;
Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA"
Matokeo ya aina yoyote yawe mazuri/mabaya hutokana na matayarisho yaliyofanywa kabla ya Jambo/tukio fulani kufanywa(kufanyika). Uwezo mkubwa/Mdogo ndio huamua Aina ya Matokeo ambayo yatakayopatikana siku za usoni za mtu.
Nikimtazama Mkulima huanza matayarisho mapema kabla ya mvua kunyesha/ kabla ya kuanza kuotesha(kupanda) mbegu akiwa na Imani kubwa atavuna mazao. Na mzao yanaweze kuwa mengi ikiwa kila hatua ya ukuaji ataichukulia hatua, mfano kupalilia, kuwekea mbolea. Matayarisho yote haya huchangia upatikanaji wa Matokeo makubwa, Ni hii hudhihirisha kuwa Mkulima amejiandaa kuvuna mazao mengi Kama hatatokea changamoto ya mabadiliko ya Hali ya hewa.
Kama ilivyo kwa Mkulima, ndivyo ilivyo kwa mwolewaji/mwowaji kuwa na matayarisho kabla ya kuingia katika Maisha ya Ndoa (Mwanzo mpya wa familia mpya). Utayari wa Akili(saikolojia) katika kuingia kwenye ndoa utamfanya mtu aweze kuwa tayari kwa ajili ya changamoto za Aina yoyote atakazo kutana nazo. Mtu wa aina hii amejiandaa kikamilifu kwa ajili ya Maisha baada ya sherehe Ukumbini.
Kuna baadhi ya watu hujiandaa kikamili kiakili, kimwili n.k kwa ajili ya sherehe ya Ndoa Ukumbini bila kujua kuwa ndoa sio tafrija/Sherehe Bali ni muunganiko wa watu wawili wanaotofautiana Fikra/upeo/uelewa wanaokwenda kujenga nyumba moja(familia). Maisha ya Ndoa ni zaidi ya sherehe, ni zaidi ya shera/suti; Ikiwa mtu anaweza kujiandaa kwa ajili ya vitu hivyo Kuna uwezekano mkubwa baada ya sherehe kuanza kuinuka kwa migogoro isiyokuwa na maana kwa kuwa kilichokuwa kwenye Ufahamu wa mtu ni sherehe na sio Maisha baada ya sherehe.
Sio kosa Wala Dhambi kujiandaa kwa ajili ya sherehe lakini ni vyema na Muhimu kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya Maisha ya Ndoa ili changamoto yoyote ikijiinua Basi iweze kutatuliwa kwa utulivu wa Akili.
Leo ukijiandaa vyema unaweza kupata Matokeo mazuri, lakini Kama hakuna maandalizi mazuri na Bora itapelekea kupokea Matokeo Mabaya.
Nafasi ya MUNGU tumpatie MUNGU mwenyewe, lakini nafasi inayomhusu mwanadamu (mtu), Basi mwanadamu aitendee Haki.
Asante.