KAMA UNACHEPUKA BASI FAHAMU HILI KWANZA!

0
Kama unatembea na mume wa mtu, hata kama unampenda vipi lakini kama anakuhonga basi huyo mume wa mtu anaamini kuwa humpendi bali unmdanga. Anakupa pesa nyingi si kwakua anakupenda au una maajabu yoyote bali kwakua anajua kuwa, kama akiacha kukupa pesa basi utamuacha.

Anawaza, kwanza nimeoa, show yenyewe mbovu, muonekano wa mashaka sasa huyu binti kanipendea nini? Anapata jibu ni pesa hata kama wewe unajiona mke, wamaana bali yeye anakuona mdangaji na anaamini kuwa, kama akiacha kukupa pesa basi utamuacha.

Sasa mwanaume wa namna hii anawaza, hivi ni kitu gani nikifanya huyu binti hataniacha milele hata kama nisipompa pesa? Anapata jibu, kama akibeba mimba yangu, nikawa na mtoto naye basi hata kama nikiacha kumpa pesa moja kwa moja hataniacha, kwanini aniache wakati nina mtoto naye.

Basi anakuambia kuwa umzalie, anakusisitizia na mwingine hata kukununulia kiwanja na kukupa mazawadi ila ukishazaa tu jua kuwa hana haja ya kukupa chochote kwakua una mtoto wake na hata ukitaka kumuacha bado una kumbukumbu yake.

Hivyo dada sanuka, mwanaume kaoa, ana mke wake,w ana watoto kibao, halafu anakuambia kuwa nataka mtoto na wewe. Yaani unajiona spesho kuwa ana mke wake halafu anataka mtoto nawewe? Unajihisi kama kizazi chako labda kina marumaru ndiyo maana anakupenda, dada, huna jipya amchoka kukupa pesa anataka uzae ili hata asipokupa pesa usimkimbie.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top