KWANINI WANANDOA WANAAMINI UONGO KULIKO UKWELI!?

0

Nagonga msumari penyewe hapa maana imekuwa ni kawaida kwa watu, hasa wale walio katika mahusiano ama ndoa kuamini uongo kuliko ukweli.
Yaani ukimwambia mtu ukweli hakuamini lakini ukimdanganya anakuamini.
Yaani hata katika mambo madogo madogo unataka udanganywe?Mke kuweza kupata fedha kwa mumewe sharti atunge uongo ndipo mume aone ni ukweli na kumpa fedha.Mume akichelewa kurudi na kutoa sababu za kweli aaminiki mpaka adanganye ndipo uamini!

Sasa mbaya zaidi hata kumpata mke ukienda na ukweli kwa binti haumpati lakini ukimdanganya anaelewa na kukukubali.Hii imefanya watu wengi kuishi maisha ya kuigiza maana wakiwa halisi hawaeleweki.

Kuna msemo usemao bora ukweli unaouma kuliko uongo unaofurahisha.Bora uumie leo kwa kuambiwa ukweli kuliko kudanganywa jambo litakalofanya uumie kesho.

Yakobo 1:14-16 inaonyesha kuwa kabla ya kufikia MAUTI kuna hatua yaani kwanza TAMAA huzaa DHAMBI,dhambi ndiyo huzaa MAUTI.

Hivyo uongo unaporundikana ndiyo huzaa matatizo makubwa zaidi ndani ya ndoa.

Mwisho kumbuka Biblia inasema ukweli ndiyo unakuweka huru siyo uongo.Kweli ni Yesu Kristo mwenywe lakini uongo ni shetani maana neno linaema shetani ndiye baba wa uongo.

Katama kweli upate kuponya ndoa yako wakati wote kama yule mwanamke aliyekamata pindo la Yesu akawa huru, kutoka kutokwa na damu kwa miaka 18(Marko 5:25-34).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top