KWANINI WANAWAKE WANADHARAU WANAUME WASIO NA PESA?✍️

0



Imekuwa mazoea kwa macho ya watu wengi lakini hii SI mazoea bali ni uhalisia. Wanawake wengi hawapendi wanaume wasio na pesa hata Kama atakupenda lakini utakuta Mara nyingi anakuuliza kuhusu malengo yako ya maisha na hakiona haueleweki anakutupa huko Kisha unaanza kulalamika wanawake wanapenda pesa. 

Hizi ndizo sababu za kwanini wanawake WANAZARAU wanaume wasio na pesa, hapa hatuzungumzii mabilionea hapana Ni wale walio na pesa na kuweza kuzitafuta zikiisha.

1: HAWANA MALENGO

Mwanaume mwenye pesa Ni mwanaume mwenye malengo ndio maana ukamkuta na vijisenti vyake ambavyo vikiisha anajiongeza kutafuta nyengine. Wanawake wanapenda wanaume au waume zao kuwa wenye malengo na malengo hayo ni utafutaji pesa na sio vinginevyo.

2: HAWANA MVUTO

Mwanaume sio sura Wala tabia MWANAUME PESA ndizo zinakupa umaridadi na mvuto hata uwe mzee, mlemavu na usioeleweka hili mradi pesa ipo inakupa mvuto au haujui wadada huwa wanahadithiana? Kuhusu wanaume zao haswa hakiwa maridadi wa fedha huvutia mno mbele za watu hata ukitaka kwenda naye mahali analeta majivuno fulani.

3: WANAKERO NA WASUMBUFU

Mwanaume hasiye na pesa ndiye mwanaume msumbufu kuliko wote duniani utamsikia kauli zake UNANIZARAU KWASABABU SINA KITU hata kama hujamzarau Mara utamsikia HAYA WE ENDELEA TU KWASABABU SINA KITU Sasa Kaka angu tafuta pesa uamkiwe na serikali sio lawama zisizo na mpango.

4: WANAVIBURI 

jamani naomba nirudie hii wanaume wasio na kitu ndio wenye viburi mwanaume anayejua kutafuta pesa hana muda wa kubishana wala kujivunia labda kwakusema HATA KAMA SINA KITU SIO UNIZARAU NAMNA HIYO 😂 Mara utamsikia hasiye na pesa MIMI SINA KITU ILA SIWEZI OMBA HATA SIKU MOJA. Sasa Kaka angu aliyekwambia Cha kwako Ni Cha kwako peke ako nani?

5: MIZINGA ( KUOMBAOMBA MSAADA KWA MPENZI WAKE)

Mnasemaga wanawake wanaomba Sana pesa ila hamjawahi chunguza wanaume wenzenu? Wanatisha kwenye MIZINGA Tena babbby kibaooo 😎 yaani acheni niwachane tu. Wanaume wasio na kitu wanaongoza kupiga MIZINGA Mara ooh baby sijui utanichoka ila tuvumiliane nisaidie Mara hii Mara ile nitakurudishia🤣🤣🤣 nikipata. Sasa utapata lini? Au ndo kikienda hakirudi.

6: WANAMISEMO MINGI

Ukitaka misemo mipya na ya zamani kwa wanaume wasio na pesa wanaongoza jamani Mara utasikia UWABATA (UMOJA WA WANAUME BAHIRI TANZANIA) yote hiyo ni misemo ya wanaume wasio na pesa.

NB: Mwanaume Tafuta pesa usije kuwaambia watoto wako V8 ni za serikali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top