Mambo 4 ya kufanya pale unapojihisi kuwa una Tatizo la NGUVU za Kiume

0

Kwa mwanaume hakuna kitu kigumu kama hiki, kuna ambao hugundua kuwa wana matatizo ya nguvu za kiume tangu wakiwa wadogo na kuamua kutokutafuta wanwake kabisa. Lakini kwa sasa kuna wengi ambao hugundua kuwa wana matatizo haya wakati wakiwa kwenye mahusiano au baada ya ndoa. Najua kama una hili tatizo ushahangaika sana na dawa, kuna wanaopona na ambao hawaponi, kuna ambao zinaisha kabisa na wengine huwa nazo kidogo. Najua ni ngumu kuishi na hili tatizo hivyo mbinu zifuatazo zitakusaidia sana kuishi kwa amani katika ndoa yako.

(1) Sio mwisho wa ndoa yako/Mwanamke anaweza kukuvumilia; Utaanza kwa kujidharau, kudhani labda mke wako taakuacha, kudhani labda atakudharau na kudhani labda ndiyo mwisho wa ndoa yako. Labda nikuambie kitu si mwisho wa ndoa yako, wanawake si warahisi kutoka kwenye ndoa namna hiyo na niwavumilivu mpaka basi. Acha kupaniki, acha kujidharau, mke wako hakudharau na kama ukiwa muwazi yupo tayari kukusaidia na kama ukijiamini hata unaweza kufurahia tendo la ndoa na nguvu hizo kidogo.

Wanawake wengi hata hawajui kama wanaume wao wana hili tatizo, huanza kujua baada ya wewe mwanaume kubadilika na kuwa na kisirani. Hapo ndipo huanza kuuliza kwa mashoga zake, kutafuta ushauri kwa makungwi na watu kama mimi ndipo anaambiwa ukweli. Ukiacha kupaniki, ukamheshimu mke wako, ukasingizia labda uchovu au ukabadilisha vyakula mke wako akawa na amani ndani ya ndoa nina uhakika atakuvumilia, hatataka kukutangaza kwakua hatataka kukuacha, manyanyaso ndiyo yatamlazimisha kutafuta msaada nnje na si upendo hivyo acha kupaniki.

(2) Acha kuhangaika na wanawake wengine wanakuchuna tu;Najua ikishindikana kwa mke wako lazima utatest nnje kuangalia kuwa tatizo ni wewe au mke wako. Ushatest mara moja mara mbili, tatizo ni wewe, nguvu zimepungua kubali na achana na wanawake wa nnje. Wanakusifia ujinga tu kuwa unawaridhisha, wanakudanganya kuwa unawapenda na ujinga ujinga mwingi ambao wanakumbia. Si kweli nikwakua wanakuchuna tu na wegine wana visirani vya ndoa. Kubadili wanawake kama nguo, kuchepuka kila siku tena waziwazi ili watu wakuoni hakukufanyi kuwa mwanaume na nguvu kurudi.

Unazidi kujitia kisirani na unatengeneza uteja wa kusifiwa kijinga jinga na wanawake. Hutakua na amani hata kama ulimwengu mzima utakuona kama mwanaume Barubaru wakati wewe moyoni ni wa dakika tano. Kwanza unajidhalilisha tu, wanajua huna nguvu sasa kwanini kujitangaza. Tulia na mke wako, ushaoa tayari wanajua wewe ni kidume. Mpe amani mke wako kusanya nguvu kidogo kwaajili yake utaona unaweza kumfikisha na kumridhisha vizuri kwakua hutawanyi tawanyi nguvu zako lakini kwakua mke wako atakua na amani na kumbuka kuwa mwanamke mwenye amani ni rahisi sana kufika kileleni kuliko mwanamke kiroho juu.

(3) Jiondolee Kisirani, jiamini wewe bado ni mwanaume;Kitu kikubwa ambacho kinavunja ndoa nyingi za wanaume wenye matatizo ya nguvu za kiume ni kisirani cha wanaume hao. Unapokua una tatizo hili kwanza unakua hujiamini, kila wakati unahisi unasalitiwa na kuona kama uadharaulika. Unaona kwakua wewe huna amani basi njia ya kumtawala mwanamke ni kwa kumnyima amani, kumtukana, kumnyanyasa na kutengeneza ugomvi usio na maana ili tu kusiwe na amani ndani na kufikia hatua ya mwanamke kuomba mechi. Hili ni kosa kwani badala ya kukusaidia inaharibu.

Kwanza kabisa wewe mwenyewe mwanaume unakua huna amani hivyo kuzidi kupoteza nguvu zaidi kwani kufanya tendo la ndoa kunahitaji na akili, kama akili yako inakisirani basi huwezi kumfikisha mwanamke. Lakini pili mwanamke anakua hana amani hivyo hata ukijitahidi kumuandaa ukimshika shika ataona kama unamuumiza tu kwakua akili yake haipo. Relx ondoa kisirani, jiamini kuwa hata kama ni dakika tano tu lakini unaweza mridhisha, mpe amani na wewe mwenyewe kuwa na amani, mwanamke anaweza kufika kileleni kwa kushikwa tu na mwanaume anayempenda kama roho yake inaamani, acha kisirani.

(4) Muandae vizuri mke wako wakati wa tendo la ndoa; Maandalizi katika tendo la ndoa ni muhimu, ukishakua na tatizo hili jua kuwa huwezi kumfikisha mwanamke kileleni kwa kufanya mapenzi tu, ile ingiza toa ingiza toa haitamfikisha. Unapokua na tatizo hili tumia muda mwingi kumuandaa mwanamke, hakikisha unajua mwili wake, unajua ni sehemu gani zinamsisimua na kuzitumia. Acha kukariri kuwa labda ni matiti, sijui na shingo hapana kila mwanamke ana sehemu yake, jua sehemu za mwanamke wako na muandae vizuri.

Kwa mwanamke kuna vilele vya aina mbili, kilele cha nnje pale kwenye kisi** na kilele cha ndani amabcho kinatokana na G-Spot. Jifunze namna ya kuzigusa hizi sehemu hata kama ni kwa dakika tano atafika. Kumbuka ulifanikiwa kumfikisha mwanamke kileleni hata kama ni kwa dakika mbili basi utakua sawa na mwenye nguvu za kiume kwani kazi ya nguvu za kiume si kulimia bali kumfikisha mwanamke. 
Mwisho nimalizie kwa kukumbushia na kurudia kuwa kinachoharibu baada ya kupata hili tatizo ni kutokujiamini, kuwa na kisirani na uoga kuwa unasalitiwa. Wanawake wengi hata hawajui kuwa mwanaume kufanya mapenzi dakika tano ni tatizo na wala hawajali. Ishu kubwa ni wao kuwa na amani, ni ngumu sana mwanamke mwenye amani kumsaliti mwanaume wake kwakua tu anafanya mapenzi dakika tano wakati ni rahisi kumsaliti kwakua anamnyanyasa na kila siku anabadilisha wanawake kama nguo.  Kama unatatizo hili zidisha mapenzi na jifunze kumfikisha hivyo hivyo na kumfurahisha utakuta wote mnakua na amani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top