MAMBO MATANO YA KUYAJUA MWANAUME ANAPOKUAMBIA KUWA MZAE KABLA YA NDOA

0


(1) Hata kama anakupenda vipi anaweza kubadilika; Inawezekana amepanga kukuoa wewe, anakupenda na kachanganyikiwa sana kuhusu wewe, lakini mambo yanabadilika, kama ambavyo alikua anampenda X wake na kachanganyikiwa juu yake na lao hayuko na wewe basi jua kuwa hata wewe anaweza kukuacha hivyo jua kuwa anaweza kukutana na mwingine akasahau kabisa kuwa alishawahi kukupenda, kama huamini muulize X wake.

(2) Ndoa si ya mwanaume peke yake; Mwanaume anaweza kukupenda, kukubali na kutaka kukuoa, lakini kwao wakakukataa, Mama mkwe akasema hakupendi bila sababu, wewe ukashangaa kumbe ni kwakua una tako kubwa, labda wewe umesoma sana, wewe kabila flani na  akasimamia msimamo wake ukaachwa kweli. Unaachwa na mwanaume anakupenda ila kashakuzalisha na ndoa huna.

(3) Mwanamke yoyote anapopata ujauzito anabadilika; hapa si zungumzii muonekano bali anakua na wasiwasi sana, maswali ya utanuioa lini, kwanini tusijenge, wivu na malalamiko ya huduma kwa mtoto yanakua mengi. Hii ni kwasababu anakua na wasiwasi zaidi ya kuachwa na mtoto kuliko kuachwa bilamtoto, wanaume wengi ambao hawajaingia kwenye ndoa wanaona kama mwanamke ana kisirani hivyo wanachepuka na kupelekea kuachana!

(4) Wanaume wengi kabla ya ndoa wanakua na wanawake wengi; Ukubali usikubali ndiyo ukweli, hata wanawake nao ni hivyo hivyo, kunai le jaribu jaribu, inawezekana wakwako hujamfumania ila mara nyingi kuna mwenzako, ubaya nikuwa ukibeba mimba mara nyingi na mwenzako naye anabeba, sijui kwanini lakini mara nyingi hatakama hawajapanga unakuta na huyo mwingine naye ana mimba na mkiwa wawili mmoja lazima aachwe na inaweza kuwa ni wewe!

(5) Zaa kwasababu unataka mtoto na si kwasababu unataka ndoa, wanaume wengi wanaotaka watoto kabla ya ndoa wanakua umri umeenda wanahitaji watoto lakini hawajajipanga kuoa, inaweza kuwa ni kujipanga kifedha au hawajaona mtu sahihi wa kuzaa naye, kuna tofauti ya nikuoe na nizalie. Anaweza kuwa alipanga kweli kukuoa lakini mambo yakabadilika, si mbaya mambo kubadilika lakini ubaya unakuja kuwa pale unapoachwa na mtoto na kubeba majukumu mwenyewe ya kulea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top