MAMBO MAWILI PEKEE UNAPASWA KUJUA KATIKA MAISHA YAKO,NI HAYA

0

MKUU WA MAJESHI MMOJA ALIWAHI KUNIAMBIA MAMBO MAWILI AMBAYO HUWAAMBIA WAFANYAKAZI WENZAKE, MAMBO HAYA, YALINIKAA SANA NA NIKAYAELEWA

Alisema ....

*1.
Kila siku kabla ya kulala, andaa sare yako na itundike Karibu na kitanda chako,

Unapopanda kitandani, iangalie sare yako na kisha jiulize.... kitatokea nini nisipovaa sare hii na nikajaribu kuingia kwenye maeneo ya jeshi?

Jibu lake ni, hakuna saluti yeyote itakuja njia yako! Kwanza utasimamishwa getini na kuulizwa maswali!

Na ikitokea mwingine amevaa sare hii hii na akapita pembeni ya mlinzi wa jeshi, hakika atapewa saluti.

Hivyo basi, saluti haikuwa ya kwako bali ni ya sare iliyotundikwa ukutani ambayo imekutengeneza lakini kumbuka, sare hiyo haitakuwa ya kwako milele! Siku moja itaenda kwa mwingine....

Kwahiyo, jiandae kwa hilo tafadhali!

*2.*
Kila siku ukimaliza kazi zako, hakikisha kila mtu ametoka ofisini kwako.

Nyanyuka kwenye kiti chako, tembea elekea upande ule mwingine, kaa kwenye kiti, na kisha kitazame kiti chako. 

Huenda kwa nafasi yako umepitisha mambo mengi sana leo ukiamini ni ya muhimu sana...

Lakini ukae ukijua, kesho kutakuwa kuna mwingine kwenye kiti hicho, na anaweza akayageuza mambo yote ambayo unadhani ni ya muhimu leo!

Mambo uliyoyapitisha, ukiamini wewe ni mtu muhimu... ilikuwa ni kiti ndo kinayapitisha na si wewe. Kiti hichi kipo kwa mda tu! Hakitakuwa cha kwako milele. Kiti hicho kimekupa mamlaka kwa mda ambapo mamlaka hayo yataondoka pale tu utakapo kiachia kiti hicho.

Tumia mamlaka hayo katika misingi ya haki,Tumia mda huo kuandika jina lako kwa DHAHABU

Tumia mamlaka hayo kuyafuta machozi ya watu wenye mazingira magumu waliopo katika jamii yetu

Tumia mamlaka hayo kujenga taifa na si kuwa na kiburi au kushehenisha ukuu wako.

*Naomba nikuulize*

Unatimia sare yako na kiti chako kufanya nini leo?

- Je unavitumia kuwakandamiza watu na kuwaonyesha kuwa wewe ndo mwenye mamlaka?  

- Unavitumia kuwasaidia washkaji na marafiki tu kwasababu wanakusifu hata pale ambapo hawastahili?

- unavitumia kugawa na kutawala na kujenga uadui? 

*- Unavitumiaje?*

- Kumbuka, mtu ambaye unamkandamiza au kumkosea kupitia sare yako au kiti chako huenda akawa msimamizi wa mtoto wako, mjukuu wako, mjomba wako,  mdogo wako au hata rafiki yako.
 

- Je utajisikiaje kama yote uliyomfanyia, yakarudiwa kwa ndugu yako?

*- Fikirini, ndugu zangu, fikirini. Kwani hakuna aijuae kesho.*

*- Tumia sare yako au kiti chako kuwaendeleza na kuwasaidia wote.*

- kuwa mama, baba, dada, na rafiki kwa wote. 

Uwe jaji mwaminifu. Sikiliza pande zote mbili za simulizi.

Muogope Muumba wako.

- Usimchukie mtu, wapende wote. Hakuna aijuae kesho,share kwa wengine wasome pia
Siku Njema.🙏🏻

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top