Mke wangu ana UJAUZITO wa mwanaume mwingine na hataki kuutoa!

0


Mimi ni kijana wa miaka 35, nimeoa na ndoa yangu ina miaka 9 sasa, lakini kwa bahati mbaya Mungu bado hajanijalia kupata mtoto. Mwanzo nilikua najua kuwa mke wangu ana matatizo, alienda hospitalini nakuambiwa kuwa ana uvimbe kwenye mirija ya uzazi, haikuhitaji upasuaji bali alipewa dawa mwisho ikaisha.

Lakini bado hakubeba mimba, basi akaenda tena kupimwa na kuambiwa kuwa yuko sawa ila bado haikusaidia, akaenda kupimwa na kuambiwa kuwa ana Hormonal imbalance ambayo aliambiwa sababu kubwa ni kutokana na msongo wa mawazo. Hali iliendelea kuwa mbaya, tulihangaika kwa miaka mitano bila kupata mtoto ndiyo wazazi wangu, nduguw engine na marafiki wakanishaauri nijaribu nnje.

Kweli nilifanya hivyo, nilikua na hamu sana ya kupata mtoto hivyo nilihangaika sana huko nnje, kila mwanamke niliyekua nikikutana naye nilikua nikimuambia kua nahitaji mtoto kwani mke wangu hazai. Nilihangaika sana lakini sikufanikiwa kupata mtoto, nilitumia pesa nyingi sana kuhudumia wanawake ili kunizalia lakini haikusaidia.

Wakati wote huo nilikua nikifanya kila kitu kimyakimya, sikutaka kumuumiza mke wangu, lakini kwa bahati kuna mwanamke nilikua natembea naye, mwaka juzi aliniambia kuwa ana mimba yangu. Kusema kweli sikuamini, nilihisi kama ananidanganya lakini baada ya kwenda kupima nilifureshi.

Nilimtambulisha nyumbani kwetu, nikamnunulia gari na kumpa kila kitu, yaani kila kitu klilikua kizuri, sikujali tena kuhusu mke wangu, ingawa sikutaka kumuambia mke wangu kuwa namuacha lakini nilimfanyia vituko vingi sana, lengo langu ilikua ni mke wangu kuondoka ili nipate nafasi ya kuishi na Mama wa mtoto wangu.

Mwaka jana yule mwanamke alijifungua, ingawa mtotio hakufanana na mimi lakini sikujali kwani alikua ni mweupe, nilimuambia kuwa nataka kuishi naye ila alikua hataki kunipekeka kwao. Kila sikua likua ananizingua, aliniambia kuwa naataka nimjengee kwanza kwakua mimi bado nina mke hivyo hataki mtoto wake kukosa urithi kama chochote kikinitokea.

Kwakua alikua na damu yangu sikuona shida, mimi sina nyumba kwani nilishakata tamaa ya maisha kwa kukosa mtoto. Nilijukua mkopo kazini, yeye alikua na kiwanaja chake, nilimjengea nyumba mpaka kukamilika lakini bado aligoma sisi kuhamiia pale kwa madai kuwa mimi bado ni mume wa mtu.

Baada ya kuona kuwa mke wangu anakua ni kikwazo nilianza mchakato wa talaka na mke wangu, nilitafuta tu sababu kuwa ananisaliti hivyo simtaki lakini ukweli nikuwa nilikua nahitaji kumuacha ili kuishi na Mama wa mtoto wangu.

Lakini wakati nikiwa kwenye mchakato wa talaka mwaka huu mwezi wa pili yule mwanamke alibadilika, alikua hataki niende kwake kwenye nyumba ambayo nilikua nimempangishia mimi, alikua hataki tuonane na nikipiga simu alikua hapokei. Nilishangaa nikaanza kufuatilia, baadaye nilikuja kugundua kuwa kumbe yule mwanamke ni mke wa mtu, ana ndoa ya kiislamu wakati mimi alinidanganya kuwa yeye ni muikristo hata jina la mtoto tulimpa la kiikristo.

Lakini nilikuja kugundua kuwa kumbe hata jina la mtoto anajingine ambalo ndiyo lipo kwenye cheti. Haikuishia hapo, ana watoto wengine wakubwa wawili ambao mimi nilikua sijawahi kuwaona, mume wake anafanya kazi darn a ndiyo anaishi na watoto kwani wanasoma huko.

Ukiwaangalia wale watoto na mtoto wangu ni kopi kabisa, nilihangaika mpaka kumfuata ofisini kwake, nilipomuuiliza aliniambia kuwa aliamua kunidanganya kwani wakati huo yeye na mume wake hawakua vizuri na mtoto si wangu kwani mimi siwezi kuzaa. Nilishangaa kwaninia nasema hivyo wakati mimi sijawahi kwenda hospitalini, niko vizuri sana kitandani ila aliniambioa hivyo mimi siwezi kuzaa kwani mbegu zangu ni nyepesi sana ni kama maji.

Kusema kweli nilihisi kuchanganyikiwa, niliamua kwenda hopspityalini kwa mara ya wkanza, kwakua mke wangua likua akienda hospitalinia naambiwa kuwa ana matatizo basi mimi nilijiona kama niko salama. Lakini hata huko nyuma kabla ya kuoa kuna mwanamke alishawahi kuniambia kuwa ana mimba yangu na nikampa pes aya kutoa hivyo sikua na shida.

Kwenda hospitalini kupima basi nikapewa jibu lilelile kuwa mbegu zangu ni maji tupu hivyo siwezi kumpa mwanamke ujauzito. Nguvu ziliniishia, nilikua nimepoteza pesa nyingi sana kwa huyo mwanamke, nilichukua mikopo mingi, kwa hasira niliamua kumtafuta mume wake na kumuambia kila kitu kuhusu mke wake lakini yule mwanamke alikua ni shetani, kumbe alikua ashampanga mume wake.

Alimuambia kuwa kuna Biashara tulikua tunafanya pamoja akanidhulumu hivyo nilishapanga kumharibia, nilitaka kumuonyesha mwanaume ushahidi lakini sikua nao, sikua na kitu chochote cha yule mwanamke, nilishapiga naye picha nyingi lakini nilipoangalia kwenye simu yangu sikua nazo hata moja, meseji zote alikua amefuta kwenye simu yangu, yaani sikua na ushahidi wowote hivyo mume wake hakuniambini na aliniambia nikae mabli na mke wake kwani mambo yetu ya Biashara hayamhusu.

Baada ya yote hayo niliona nimeshindwa, niliamua kurudi kwa mke wangu ili kuomba msamaha kwani nilishamdhalilisha sana kuwa hazai. Lakini shida inakuja hivi, nimerudi kwa mke wangu na nimekuta ni mjamzito, ameniambia kabis akuwa alipoona kuwa mimi nina mtoto na mtu mwingine na nataka kumuacha aliamua kuchepuka na amebeba mimba ya mwanaume mwingine.

Kusema kweli nimechanganyikiwa, mke wangu ana ujauzito ambao najua ni wa mwanaume mwingine, hajali kabis akuhusu mimi na ananiambia kama ni kumuacha nimuache lakini hawezi kutoa hiyo mimba. Bado nampenda, sijui nifanye nini, nikubali kulea tu hii mimba ya mke wangu ili kukwepa aibua u nifanye nini? Vipi |Baba wa huyo mtoto kama ikitokea akija kudai mtoto wake si nitaaibika, naomba ushauri wako sijui chakufanya kabisa!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top