Mke wangu kakasirika X wake anaoa,nimegundua anaomba warudiane.

0

Habari naomba ushauri wako, mimi ni Kijana wa miaka 33, nimeoa ndoa yangu ina mwaka mmoja na nusu sasa, kabla ya kukutana na mke wangu alikua na mwanaume wake, walikua na mahusiano ya muda mrefu lakini mimi nilimpenda, nilimshawishi mpaka akaachana na yule mwanaume kwani niliona kama vile hampendi.

Mwanaume alikua ashamtambulisha kwao lakini alimkataa na sisi tukafunga ndoa ya harakaharaka, mwanzo yule jamaa alitusumbua sana lakini baada ya kupata mtoto aliacha kutusumbua akaendelea na maisha yake. Maisha yaliendelea, lakini sasa hivi kuna kitu kimebadilika, yule X wa mke wangu anataka kuoa, naona mke wangu kabadilika, amekua ni mtu wa hasira sana, amekua ni mtu wa kutukana.

Mimi nahakikisha anapata kila kitu, lakini anahangaika na mchumba wa X wake, anaweza kumpigia simu na kumtukana, anamtumia ma meseji ya matusi huku akimuambia kuwa pamoja na kwamba mwanaume anamuoa lakini anampenda yeye. Anahangaika kumtumi yule mwanaume meseji za matusi akimuambia kuwa hata akioa basi hawezi kuwa na furaha.

Mimi nilikasirika na kumfuata jamaa nikamuambia kuwa kama anoa kwanini anahangaika na mke wangu. Hapo ndipo nilichoka kwani alinionyesha meseji nyingi akimuambia mke wangu kuwa apambane na ndoa yake asimsubue lakini mke wangu ndiyo hataki. Ashamblock mara kibao ila mke wangu anaendelea kumtafuta na kumtumia mapicha ya hovyo.

Mimi ndoa yangu haina amani kabisa, yaani ni kama mwanamke bado anampenda X wake, X wake hana habari naye, nikimuuliza mke wangu ananijibu majibu ya dharau ananiambia niamue ninachotaka yeye hajali. Niko njiapanda, mke wangu nampenda kuliko kitu chochote, nimempa kila kitu lakini haridhiki, naona kama huyu X ndiyo anamchanganya, hatuna amani, mke amekua ni mtu wa kunywa pombe hata mtoto hajali.

Mabinti wa kazi anafukuza kila siku inanibidi mimi nitoke kazini kumuangalia mtoto kwani nikiacha anaweza kukaa kutwa nzima hamlishi au akaondoka nyumbani na kumuacha wakati mtoto mwenyewe mchanga, nikimuuliza anasema nitajua mwenyewe niamue.

Ni kama anataka nimuache, nashindwa kuelewa kwani mwanzo tulikua vizuri ila baada ya kusikia X wake anaoa ndiyo kawa kama kachanganyikiwa mpaka nahisi labda jamaa kamloga ili sisi tusiwe na amani, naomba ushauri wako nifanye nini?

JIBU LANGU; Ulimharakisha sana mke wako kuoana naye kabla ya kumsahau X wake, yaani ulipaswa kumuacha aumie kwanza na kukubaliana na ukweli kuwa hapendwi na huyo mwanaume ndiyo uanzishe mahusiano naye, lakini wewe ulimharakisha. Hilo lilikua kosa la kwanza, kosa la pili ambalo unalifanya sasa hivi ni kumuonyesha mke wako kuwa huwezi kuishi bila yeye. Hili ni kosa kubwa, mwanamke akijua kuwa anaweza kukufanyia vituko vya aina yoyote ile lakini huwezi kumuacha basi utaisoma namba.

Kama unavyoona, huyo jamaa alikua aikimnyanyasa, anamfanyia vituko lakini alikua anamng’angania. Najua unajiuliza hivi alimpa nini mke wangu, wakati mwingine unawaza labda kitandani alikua vizuri na wewe humridhishi. Ukweli nikua huyo jamaa hakua na kitu kingine cha maana zaidi ya manyanyaso ambayo yalimtengenezea mke wako Uteja.

Niamini nikimuambia kuwa wanaume wengi wanaoongoza kunyanyasa wanawake, kudhalilisha na kung’anganiwa kitandani ni sifuri na wanang’ang’aniwa kwakua wanajua kuwafanya wanawake mateja. Sasa nini cha kufanya hapa, kwanza muite mke wako, unaweza kumtoa out, muambie kabisa kuwa unampenda lakini huwezi kuvumilia mambo anayoyafanya, muambie kuwa unajua ulilazimishia ndoa ya mapema kabla hajapona lakini kamwe huwezi kuvumilia aendelee kufanya ujinga anaoufanya.

Baada ya hapo kistaraabu kabisa muambie kuwa, bila kukuomba msamaha umeamua kumsamehe lakini kama siku akilogwa akawasiliana na huyo mwanaume au mchumba wake hutaitisha kikao tena. Najua hatakusikiliza anaweza hata kukujibu kwa dharau akiamini kuwa wewe ni Kiazi huwezi kumuacha, ila usijali, ukishamaliza muambie hutaita kikao kingine na hutalalamika tena.

Najua atarudia, hataacha, basi ukishaona bado anafanya hivyo, mchukue mrudishe kwao, chukua mtoto wako lea mwenyewe. Sisemi umuache, hapana ila mpe muda wa kuwa peke yake, mpe muda wa kuona umuhimu wake, mpe muda wa kuchanganyikiwa kidogo. Ukimrudisha kwao hakikisha huongei na mtu yoyote, usimpe Talaka lakini muambie huwezi kuongea na mtu tena ushamaliza.

Rudi kwako, kaa kimya, usimtafute tena, hata akikupigia usionyeshe hasira ongea kuhusu mtoto na si kingine. Kaa miezi mitatu, huyo mwanamke asiporudi si wako alikua hakupendi alifanya makosa kuolewa na wewe lakini akirudi mpokee na atakua amejifunza usikumbushie makosa ya nyuma na hata siku moja hutasikia akiwaisliana na X wake.

Hapa ni umafanya mambo mawili, moja umemfundisha kuwa unaweza kumuacha na maisha yako yakaendelea, ukamuonyesha umuhimu wako lakini pili umempa kipindi cha kuumuia, kutafakari, kujua maisha yakoje na kuwaza kama anakuhitaji au la. Klipindi hiki kama hutaonyesha kumshobokea huyu mwanamke atafahamu umuhimu wako na utakua na amani sana katika ndoa yako, pia nawe utajifunza kuacha kumng’ang’ania mwanamke.

MREJESHO; Itoshe tu kukuambia ndugu yangu kuwa, nilifuata ushuari wako, mwanzo niliona kama ni wakipuuzi lakini nilipoona mke wangu kamtumia picha za uchi X wake niliamua kumrudisha kwao. Huyu mwanamke ni mjeuri, alikaa miezi sita kwao, mtoto niko naye mimi, sikumtafuta wala kuhangaika naye mpaka alipokuja huku, akilia, nilishakata tamaa lakini nilimsamehe na sasa hivi nina amani.

Kusema kweli kabadilika sana lakini hata kama singebadilika kipindi hiki kimenifundisha kua naweza kuishi bila yeye. Hata mimi nilikua kama mwehu kwake, namng’ang’ania lakini sasa hivi mambo ni toafauti. Alikua ananikosea namuomba msamaha mimi ila sasa hivi hata akinuna mashavu yakalegea mpaka kugusa sakafu sijali na msamaha anomba, nashukuru nimekua na amani tena sana.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top