MUME WANGU ALINIAMBUKIZA UKIMWI NA KUNIACHA KWAKUA NAMPA STRESS

0


Mimi ni binti wa miaka 23, nimeolewa na ndoa yangu ina mwaka mmoja sasa, kabla ya ndoa mimi na mume wangu tulikaa kwenye mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja tu. Kipindi hicho ndiyo nilikua nimemaliza chuo Diploma na bado nilikua sijapata kazi. Mume wangu ni mtu mwenye pesa zake, yeye ana miaka 32 kanizidi miaka tisa. Mwanzoni sikujua tabia zake lakini kabla ya ndoa niligundua kua ana wanawake wengi sana.

Alishaoa na kushindwana na mke wake ambaye walizaa mtoto mmoja mwanamke akakiambia kutokana na umalaya wake. Mimi alinificha na nilipogundua nilitaka kuondoka, niliwaambia nyumbani na kusema sitaki ndoa. Alikuja kuomba msamaha na kusema kabdilika lakini bado nilikua nikifumania meseji akawa ananiambia atacha umalaya taratibu. Ndugu zangu walishikilia kidete, dada zangu ambao wapo kwenye ndoa walikua wakiniambia wanaume wote wako hivyo.

Waliniambia ilimradi pesa ananipa na ananihudumia basi nivumilie atabadilika. Nilikataa katakata lakini viliitishwa vikao vingi na kuwa kama nalazimishiwa, walinishawishi mwishoe nikakubali tukafunga ndoa. Lakini baada ya kuingia kwenye ndoa sijawahi kufurahia ndoa hata siku moja, mwanaume hawezi kulala na mwanamke mmoja, kila siku nikubailisha na anarudi nyumani anataka nimpe unyumba, nikikata anakasirika na kunipiga, nilirudi nyumbani lakini hawakujali wakaniambia vumilia.

Nilivumilia kweli Kaka Iddi lakini ndoa yetu ikiwa na miezi nane, nilisikia tetesi kua mume wangu anatembea na Dada mmoja ambaye alikua ni muathirika, nilikua na wasiwasi sana na kuamua kwenda kupima. Nilipima na kukutwa kweli nimeathirika, mwanzo niliona kama utani lakini nilipopima tena niliambiwa nimeathirika, nilienda kimya kimya na nilipokutwa ninao nikamuambia mume wangu na kumuomba nayeye akapime kwani sijawahi kuwa na mwanaume mwingine katika maisha yangu yote ni mwanaume wangu wa kwanza mpaka ndoa.

Mume wangu alikataa kupima akaniambia yeye hana na mimi nampa stress tu. Alinifukuza kwake na hataki tena mawasiliano na mimi, nimerudi kwetu ndugu baada ya kusikia nimethirika wamenitenga, sina kazi lakini hakuna anayetaka kuishi na mimi, wananirusharusha kama mpira, hawataki hata niwabebe watoto wao hata chakula hawataki kula pamoja na mimi. Niko njia panda Kaka nimechanganyikiwa kwani mume hataki kunisikia na ndugu zangu ambao nilikua na wasaidia hawataki hata kukaa meza moja na mimi sijui nifanye nini?

JIBU LANGU; Kila kitu kinachotokea kwenye maisha kina sababu, huwezi kujikinga kwa asilimia mia moja. Ni kweli ulipogundua kuwa anachepuka tena na mtu aliyeathirika ulipaswa kusimama na kusema hapana, siwezi kuhatarisha maisha yangu namna hii. Lakini Dada hata sikulaumu, baada ya kuongea na watu wengi wanaopitia hali kama yako nikuambie tu ukweli nikuwa ni ngumu sana kwa mwanamke kutoka katika mateso kuliko kutoka katika starehe.

Dada umeathirika lakini hujafa, miaka ya nyuma UKIMWI ulikua ni sentensi ya kifo, kukonda, kuteseka na kila kitu. Lakini sasa hivi kuna dawa za kutumia, unakua sawa kabisa na nikuambie tu kuwa huko mbele wazungu hawalali wataleta tu dawa sasa kuliko kukata tamaa na kufa kwa mawazo ishi kwa matumaini, kuna watu kibao wapo kwenye hali kama yako na maisha yanaenda tena raha mstarehe, acha kuumiza kichwa sana.

Dada kuhusu ndugu zako achana nao, una mikono miwili na miguu miwili,a mua useme hivi, hawa wanaonitesa leo hii watakuja kwangu wakiwa CHAWA, elekeza nguvu zako katika kutafuta pesa, tafuta kazi yoyopte, jishughulishe na kasirikia huko, ukielekezea nguvu zako huko kwanza mawazo yatapungua, utakutana na watu wapya lakini baada ya muda ndugu wataanza kukuona wa maana utawacheka tu, Dada fanya hivyo uje unipe mrejesho hapa, ukikwama nicheki, simu yangu iko bize sana usikate tamaa kunitafuta ila usijafanya maamuzi yoyote bila kuongea na mimi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top