NAMNA YA KUISHI NA MWANAUME MCHEPUKAJI

0

Kuna wanawake ving’ng’a nizi mpaka unaanza kufikiria wana kasoro gani, labda ni pesa zinawaweka au ni ile hali ya kutokujiamini. Kwamba wanajidharau vyakutosha kiasi kwamba wanaona wakiondoka hawawezi kupata mwanaume mwingine.

Lakini kwa bahati mbaya zaidi wanawake hawa wanaamini kuwa maisha bila mwanaume si maisha. Kwamba kwao ni bora kuchangia mume, kupigwa na kunyanyaswa kuliko kuishi peke yako kwa amani.

Sasa kwa mimi ukiniuliza kuhusu mwanaume anayechepuka ningekuambia tu hembu ondoka, kama umemsamehe zaidi ya mara tatu na ndiyo anazidi basi kwa usalama wa afya yako, kabla hajakuletea UKIMWI ondoka.

Hakuna namna ya mwanaume wa namna hiyo atabadilika, sijui nyie ambao mnaamini katika maombi ila kwa sayansi ya kawaida kama akikusaliti mara tatu basi ukimsamehe tena jua ndiyo tabia yake si wakubadilika.

Sasa kama wewe ni kichwa maji hutaki kukubali kuwa habadiliki, umesema poteli ya mbali naishi naye huyuhuyu, sasa hembu nikusaidie kidogo juu ya namna ya kuishi na mwanaume wa namna hii.

Hapa sio kwamba utambadilisha, hapana lakini angalau utakua na kaamani kidogo, utakua na furaha na maisha yataendelea. Hapa haijalishi kwanini huondoki, labda ni pesa, au upendo lakini labda hutaki tu kukaa mwenyewe mbinu zifuatazo zitakusaidia.

(1) Acha Kumfuatilia; Sijui hata unamfuatilia nini, unajua anachepuka lakini kila siku umeshikilia simu yake, uanasoma mesji na picha alizotumiwa. Unawekeza katika kumfuatilia yeye kuliko kuwa na furaha, ninachoona ni kama tu unataka kujilinganisha na hiyo michepuko yake uumie useme anakuumiza!

Mama unajiumiza bure, ushajijua huondoki sasa unataka nini, yaani ni sawa na kuweka mkono kwenye maji ya moto, wakati unajua ni ya moto utaungua bure.

Hivyo kama umeamua kubaki, kama ushamfumania mara tatu na ukamsamehe acha kumfuatilia acha kuahangaika kuwa kwanini kachelewa, alikua na nani, alisimama na nani, simu ya nani na ujinga ujinga mwingine kama huo.

Wewe kama una kaimani mauchie Mungu na acha kumfuatilia. Labda nikuambie kitu kingine wakati mwingine wanaume wa namna hii hata si wazinzi sana lakini kila unapomfuatilia na kuonyesha kujali ndiyo anapata mzuka wa kuchepuka zaidi.

Lakini kama hufuatilii tena ataanza kuona anachofanya ni utoto atapunguza au hata kuacha kabisa. Najua ni ngumu lakini jitengenezee utamaduni huo, siondoki na sikufuatilii, anayofanya nnje ya nyumba yako hayakuhusu.

(2) Dharau Na Puuzia Michepuko Yake; Nakushanga eti unaupigia mchepuko wa mumeo simu , mnatukanana na kumuambia kuwa wewe ndiyo mke halali, sijui unapendwa sijui nini.

Mama anayajua yote hayo na lengo lake la kupiga simu usiku ni ili kuwagombanisha, anajua ana mke na wala hajali hata kama ukimuambia una UKIMWI hata dharau ashajipanga muda mrefu na matusi yako na maneno yako, kitu cha kufanya ni kuidharau.

Anapopiga simu usiku wala usijifanye kukasirika, unaweza kupokea nna ukamuambia onge ana mwenzio. Yaani hapo atajiona kinyaa na akiona kama hustuki na wewe huondoki ndiyo atajiona mpuuzi.

Lakini jinsi unavyotukana ndiyo unavyompa mzuka wa kuzidi kumshikilia mumeo, yaani wanadamu tuna kitu cha kiushindani ndani yetu, kwamba kwanini yeye aolewe, ana uzuri gani?

Wakati mwingine atataka kukuharibia ili mkose wote hata kaama akijua kua haolewi. Hembu jaribu kuipuuza, wala usijali, usionyeshe kukasirika, hakuna adhabu kubwa kama dharau ya ukuta. Kwamba unaupiga ukuta ngumi lakini wala haukurudishii.

Kuwa ukuta, wakipiga simu, ukikutana nao na wakaijifanya kua wapo juu shuka na waulize mmemaliza. Tena akikupigia simu mjibu kistaarabu lakini kwa dharau flani kuonyesha kama hujali.

“Mama wewe si unamtumia, mbona akirudi mzima kabisa kama alivyoondoka, kingekua kinapungua ndiyo ningepata presha kuwa kitaisha lakinisasa walaa wewe tumia tu, na kama ni UKIMWI mpe mimi nitauguza wala usijali” hapo utaona kama atakutafuta tena na wala hutaumia tena.

(3) Tafuta Hobi; Ndiyo tafuta kitu cha kukupa furaha cha peke yako, kitu cha kukuondolea mawazo, kitu cha kukufanya usimuwaze sana. Wengine hutafuta michepuko, hili sikushauri, madhara yake nitakueleza iisku nyingine.

Lakini kumbuka kua mumeo hata kama ana michepuko mia akikukuta na mmoja anakutimua hivyo kama umeamua kubaki vumililia na kama umeamua kuchepuka basi jua ukikutwa unaachwa, usiniulize kuwa sio haki lakini ndiyo hivyo.

Sasa tafuta kitu cha kukuondolea mawazo, tafuta hobi, labda kuangalia muvi, mazoezi, kutoka out, na vitu vingine ambavyo vitakupa furaha na kukuondole mawazo, vitu ambavyo vitakusaidia kupunguza kuwaza.

(4) Tafuta Kazi ya Kufanya; Ndiyo kama una kazi basi hongera, wekeza kaili yako katika kazi, kama huna basi anza kutafuta. Lakini hapa inawezekana hataki ufanye kazi, simama na muambie hapana.

Huwezi kuwa na haki ya kuchepuka halafu bado ukawa na haki ya kunikataza nisifanye kazi, muambie kuwa kama unachepuka ipo siku utaniacha na sitaki niende kuwa ombaomba kwa ndugu zangu.

Kama anachepuka na anakukataza kufanya kazi halafu bado ukakubali ukaka abasi na wewe una matatizo unahitaji maombi ya muda mrefu kwani hujitammbui. Si una miguu na mikono kwani ukiondoka ukianza upya utakufa, fanya kazi.

(5) Fanya Uwekezaji Binafsi:  Mwanaume akishachepuka. Hasa wale ambao huonyesha waziwazi, yaani mpaka huo mchepuko wake unakupigia simu jua kuwa hata kama hutaki kuondoka kuna uwezekano mkubwa ukatelekezwa.

Ndiyo kwani huo mchepuko unaweza kukupindua wakati wowote na mumeo aissieme chochote. Sasa maumivu ya mapenzi ni mabaya na huuma, ila huuma zaidi pale ambapo unaaachwa halafgu unaenda kuanza moja.

Huna hata kijiko ni kulialia tu, unaenda kuwa mzigi kwa ndugu. Kwa maana hiyo basi kama uko katika hali hii anza kuwekeza kivyako, huu ndiyo wakati wa kununua kakiwanja kako, ndiyo wakati wa kuanza kujenga na kufungua kabishara kako.

Ndiyo unatakiwa kuwa na chako, nakuhakikishia mwanaume akikuacha ukiwa na pakwenda inanafuu kuliko unaachwa halafu na watoto wako watatu mnaenda kwa kaka yako kuishi kumsumbua wifi yako.

Acha kubweteke kuwa nakupenda kama anachepuka hakuna cha upendo wala baba yake upendo mpompo tu kwa kudra za Mungu wekeza kila senti unayoipata kwajaili yako na akigunuda muambie naogopa kuachwa.

(6) Husika Katika Miradi Yake Ya Maendeleo: Kuna wanawake wengine wapo ndani ya nyumba utafikiri wao ndiyo wa dada wakazi, mue ana nyumba hajui hata hati ina jina gani. Ana biashara hajui hata inaendaje, mume anaunua viwanja hujui kamuandika nani.

Yaani umechunguza mpaka umejua kuwa anachepuka lakini unashindwa kuchunguza kujua kuwa ana kiwanja. Labda nikuambie kitu kimoja michepuko yake inajua na inachunguza.

Sasa kama ni ile michepuko mijanja yenyewe inajua wakati wowote inaachwa hivyo inachuna vyakutosha. Ukiwa mjinga utadhulumiwa kila kitu, hivyo ukihisia nachepuka basi kuwa makini na mali mlizochuma.

Kama kuna kiwanja chenu hakikisha kina majina yenu au ya watoto na akitaka kuuza basi uwepo na kupinga kuwa hawezi kuuza au kuabdilisha hati kwakua ni vyenu wote.

Wewe zubaa tu useme unamuchia Mungu, tayari Mungu kakupa akilia na uzima unataka nini tena aje akupeleke kwenye kiwanja kilichaonunuliwa, akili ile ile iliyokufanya ujue michepuko yake ndiyo hiyo ikufanye ujue kuwa anajenga wapi na nyumba ina jina la nani.

Komaa vitu viwe na majina ya watoto na kuwa makini ujue anamiliki nini na nini. Kuna leo na kesho hivyo usiangalie tu kulia mapenzi sijui nimetendwa, si umemaua kubaki baki kijanja.

Mwisho nimalizie kwa kusema mapenzi ni changamoto lakini kama umeamua kukabiliana nazo kabiliana nazo acha kulalamika. Sio unabakia halafu kila siku unalialia kwa marafiki.

Hao wenyewe unaowalilia nao wana matatizo yao, hivyo kama mume amekusaliti mara tatu huyo habadiliki, hata ukinywa mikojo kama chai bado ataendelea kuwa vilevile nilazima uamke na kuangalia maisha yako kwani kashakuonyesha dalili kuwa anaweza kukutimua wakati wowote.

Nimalizie kwa kusema, furaha ya ndoa yako unaitengeneza wewe mwenyewe. #HAKUNAKULIA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top