NASAA ZANGU 10 KWA WANAWAKE USIPITWE ZITAKUSAIDIA TAFADHALI.

0


 1. Mwanaume atakaekutambulisha kwa wazazi wake na si kwa rafiki zake pekee huyo ndiye mwenye mwelekeo wa kufanya maisha na wewe.

2. Usitizame gari wala pesa nyingi ukadhani ndio kipimo cha utajiri wa mwanaume, ndoto na maono yake yenye tija ndio muelekeo mzuri wa utajiri wa mwanaume.

3. Ni wazi kwamba mwanaume anaweza akakupa talaka au kukufukuza kwake, ila elimu, ujuzi na kipaji hakiwezi kukupa talaka. Hivyo basi focus katika kupata elimu na ujuzi kabla hujampata mwanaume wako.

4. usikubali zinaa ikufanye kuwa mama kabla ya ndoa kukufanya kuwa mke. Tangulia kwanza kuwa mke ndipo uwe mama.

 5. Wanaume bora sio vigumu kuwapata, ila ni vigumu kuwavutia. Hivyo basi kama unataka mwanaume bora jiandae kumvutia. Si kumvutia kimapenzi! La hasha binti yangu..namaanisha kuwa na tabia na siha njema anayokufunza mama yako na dini yako 

 6. Matokeo ya kuwadharau wanaume walio bora wenye dini na hofu ya Allah na kujichanganya na wanaume matapeli ni kwamba utakuja kuchanganyikiwa, hasira na visasi pale utakapoona wale wanaume bora uliowadharau wanaoa wanawake ambao nao uliwaona kama sio wazuri kama wewe.

7. Usijiaminishe na kujiachia katika uchumba na mahusiano mengine ya haraam wakati Amesema Mtume swala Allahu 'alayh wasalaam," tangazeni ndoa na uchumba"

 8. Jipende na ujitunze, ni msiba kuona Allah amempa thaman mwanamke hata kwa kuonesha mwanamke Ana thaman kiasi gani Allah akaamrisha ufunikwe mwili wote wa mwanamke kwa kuonesha Una thamani kubwa kiasi gani
 
10. Hakuna mpumbavu mkubwa kama mwanamke ambae anamdharau mwanaume kwa sababu ya hali yake ya kiuchumi aliyonayo kwa wakati huo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top