Kama unamuamini sana Mama yako unatakiwa kukumbuka kuwa ni mke/alikua mke wa Baba yako, inawezekana Baba yako hakuwahi kumuamini lakini kwako ni mwanamke muhimu sana. Lakini kama humuamini mke wako kumbuka kuwa ni Mama/atakua Mama wa watoto wako na wanao watakuja kumuamini kama unavyomuamini Mama yako leo.
Hivyo kama una imani ya kweli na Mama yako kuwa anakupenda na hawezi kukufanyia baya lolote, basi unapaswa kumuamini mke wako na kuamini kua anawaenda/atawapenda wanao na hawezi kuwafanyia baya lolote. Huwezi kusema unampenda Mama yako na kumshirikisha katika kila kitu unachofanya wakati humpendi mkeo na humshirikishi kwa chochote.
Kumbuka unapoamua kuanza familia huishi kwaajili ya leo bali ya kesho pia. Kwa maana hiyo ili kesho ya wanao iwe salama ni lazima Mama yao awe salama, kwani mwisho wa siku huyo mwanamke unayemuita mkeo leo, uwe unampenda au humpendi, uwe unamjali au humjali ndiye atakua mwanadamu muhimu kuliko wanadamu wote kwa watoto wakom mtunze!