Nifanye nini? Wifi yangu anamchuna sana Kaka yangu

0


Habari Kaka, mimi ni binti wa miaka 29, sijaolewa na sipo kwenye mahusiano kwa sasa, nina mtoto mmoja, naishi kwa Kaka yangu ambaye yeye ni Mwanajeshi ameoa na ana watoto wawili. Mwanzo mimi na wifi yangu tulikua vizuri kwani kuna mwanaume nilikua naishi naye alikua ananinyanyasa na nilipokuja alinipokea vizuri.

Mwanzoni kwakua walikua wanaishi pamoja sikuona tatizo, lakini baada ya mwaka jana Kaka yangu kusafiri ndipo niligundua unyama wa wifi yangu. Kaka yangu ni mwanajeshi, na ana cheo kikubwa tu, anasafiri nnje sana na sasa hivi yupo nnje kikazi kwa mwaka sasa. Tatizo ni kwamba anamuamini sana wifi kiasi kwamba msahara wake wote yeye ndiyo anachukua kiasi kwamba eti tukitaka matumizi mpaka tumuombe yeye. 

Haiishi hapo, Kaka anabiashara basi zote anasimamia mke wake, mimi nina ndugu wa kiume hawashirikishwi kabisa. Lakini kitu ambacho kimenifanya niulize nikuwa, kuna wakati Kaka alituma pesa flani, akamuambia wifi kununua kiwanja, wifi alinipeleka mimi kama shahidi, kufika nikakuta kaandika jina la mtoto.

Mimi nikashtuka na kumuuliza kwanini haandiki jina la Kaka wakati yeye ndiyo katoa pesa akasema wamekubaliana kuwa vitu vao wote kuandika watoto. Nilishtuka na kuanza kufuatilia, kaka kumbe wana vitu vingi, nilikuta hati za viwanja kama saba hivi ambavyo sisi kama ndugu hatuvijui lakini hakuna hata kimoja kina majina ya Kaka, vyote vina majina ya watoto, naomba nisaidie ni kwa namna gani nimuambie Kaka yangu kuwa anaibiwa!

JIBU LANGU; Ungekua ni Dada yangu ningekua nishakufukuza kwangu kwakua hapo unachowaza ni “Kaka yangu akifa mali zitabaki kwa nani?” Ngoja nikuulize hivi siku Shangazi zako wakija na kuanza kuulizia mali za Baba yako mtakaa kimya au mtaongea. Huyo wifi yako tena ni Jembe, yaani anaandika watoto wake bado unaona wivu!

Nikuambie kitu, muombe Kaka yako mtaji, anza Biashara kisha ondoka hapo acha kuhangaika na mali za Kaka yako, si zako, narudia si zako na hazikuhusu. Wewe Kaa hapo ukiomba Kaka yako afe ili mgawane mali mpaka unashtuka ushaota MBELEWELE unanyauka huna hata chumba cha kulala!

Najua unamuonea wivu wifi yako kwakua wewe Mume wako alikua anakupiga, anakunyanyasa hakupi kitu. Kuna wakati unawaza hivi huyu ana nini cha ziada ambacho mimi sina, nikuambie chaziada alichonacho nikuwa yeye anaongea na Kaka yako wakiwa kitandani wewe unaongea naye sebuleni, yeye kamzalia Kaka yako wewe wewe unamjazia choo Kaka yako, yaani hata kama asingezaa ni mke wake wewe ni dada yake!

Ndugu yangu, omba mtaji ondoka achana na mali za Kaka yako!
\

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top