Nilikua natembea na MUME wake, amekufa anataka nirudishe pesa zote nilizomchuna!

0Kaka mimi nisaidie, kuna mada umeandika jana kuhusu mwanaume ambaye anamtumia Dada kwakua kachukua picha zake za uchi. Kaka mimi ishu yangu ni tofauti, mimi nimeolewa ila nilikua na mchepuko wangu wa muda mrefu hata baada ya kuingia kwenye ndoa bado niliendelea naye. 

Mke wake nilikua nagomambana naye sana lakini mwaka jana kwa bahati mbaya yule mwanaumealifariki dunia ndiyo tukaja kuachana. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, nilimuambia huyo mwanaume kuwa nina mtoto naye na akawa anahudumia kama wake ingawa alikua akitumia jina la mume wangu, sasa yule Mama ni mtu mzima ananitishia kumuambia mume wangu kila siku.

Ana cheti cha cha kuzaliwa na simu ya mume wake anajua kila kitu, mule kuna picha zangu nyingi za uchi ambazo nilipiga na mume wake, meseji ambazo nilikua nikichart naye hivyo ananisumbua na kuniambia kwua niwe nampe pesa kwani yeye maisha yake ni magumu hivyo anataka niwe namsaidi akulipa ada za watoto wake la sivyo atamuambia mume wangu.

Kaka mume wangu namfahamu, ananipenda sana na si mchepukaji, yaani ni yule mtu akijua kuwa nilikua namsaliti hanipigi ataniacha tu bila kuongea kitu. Alishaniambia kuwa tukishindwana hataki mambo ya kusuluhishwa wala nini, alishaniambia kuwa hatanisaliti kamwe na kama kuna mapungufu nimuambie ila hataki mambo ya kusalitiana, yaani Kaka nahisi kuchanganyikiwa.

Yule watu walimuambia aende Polisi lakini Kaka nikienda Polisi mume wangu akijua kua nilichepuka tena na mume wa mtu na mtoto alikua analea sijui kama atanisamehe anampenda sana mtoto ambaye anajua ni wake tuna watoto wawili, mmoja ni wa mume wangu mwingine ni wa huyo Baba. Naomba unisaidie kwani huyu Mama naona kama anataka kuniua, ananiambia yeye hakua na maani kwenye ndoa yake kwajaili yangu hivyo ni zamu yengu kurudisha pesa za mume wake nisaidie Kaka nifanye nini?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top