Habari kaka naomba ushauri wako tena, nilikutafuta mwaka jana kuhusu mume wangu, wakati huo ndoa yangu ilikua na miezi sita na nilikuambia kuwa mwanaume wangu yeye ni mtu wa marafiki, yaani ukismahauri kitu hakusikilizi aasikiliza marafikii na ndugu zake. Ana Biashara nyingi lakini mimi kama mke wake sijui chochote anafanya na dada yake.
Nakumbuka uliniambia nimeanza mapema kudai urithi kana kwamba wmanauem anakufa kesho. Niwe mpole na nisiulize kuhusu mali zake tena kwania takuja kuniambia taratibu. Uliniambia kuwa mume wangu kwasasa haniamini, si kwakua nimsheni au hanipendi bali kwakua hajanizoea, watu wanawaamini watu wanaowajua kuliko wageni.
Niliumia sana kwani mimi ni mke wake lakini nila kitu alikua anafanya na dada yake, uliniambia kuwa Dada ni Shangazi tu atapita ukaniambia niake kimya niwe bize na kazi yangu na Abdala ya kuhangaika na Biashara za mume wangu basi nihangaike na kufungua Biashara zangu.
Kaka nilikusikia lakini kila nilipokua naona kama wifi yangu anatawala roho iliniuma sana. Nilishindwa kuvumilia, nikawa nachunguza kila kitu cha mume wangu kutaka kujua kwani nilijua kama kikitokea cha kutokea hapa siondoki na kitu. Nilihangaika kufuatilia, nikawa naenda dukani mabapo alimuweka mdogo wake, tunagombana sana lakini sikujali nilikua napigania haki zangu.
Mwaka huu nilibeba ujauzito, hapo ndipo niliona kabisa kuwa dunia imeisha kwani nilijua na mtoto kama mume wangu akifa basi itakua shida kwangu kulea mtoto kwani kila kitu anafanya na ndugu zake. Katika kuhangaika kuna rafiki yangu aliniambia mume wangu hayuko sawa, kuna asilimia kubwa kuwa ndugu zake wamemtengeneza hivyo na mimi natakiwa kujipanga.
Alinishauri kwenda kwa mganga ili kuangalia, kwakua nilikua na mawazo mengi kweli nilienda Kaka na ilionekana Mama yake ndiyo anamshikilia, amemtengenza kwelikweli. Nilipewa dawa. Nikwa natummia, mwezi uliopita mume wangu alinisikia naongea na simu, kuna dawa nilipewa kwaajili ya kumuwekea, basi akanisikia.
Alikaa kimya lakinia lichukua namba ya Mganga niliyekua naongea naye, akajifanya kwua ana shdia, alimfuatilia mpaka kumpata, mume wangu ni Mwanajeshi, alichofanya Kaka alichukua wenzake mpaka kwa huyo Mganga walichomfanyia sijui ila aliongea kila kitu, wakaniwekea mtego nikienda kuchukua dawa kule kwake, basi mwanaume alinifukuza mpaka leo hataki kurudiana na mimi kwa madai kuwa nilitaka kumloga.
Kaka mimi sikutaka kumloga bali niliona kama anashirikisha zaidi ndugu zake. Kaka nina ujauzito lakini hanitafuti hata kuniulizia kama ninaendeleaje, nimejaribi kuomba msamaha lakini hataki hata kunisikia. Nisaidie kaka nifanye nini, sikua na niambaya, najua uliniambia ninyamaze lakini kaka nilishindwa na sasa hivi sijui nifanye nini kaka?
Like share comment