Nimebeba MIMBA ya mume wa mtu kumbe naye ni CHAWA tu!

0

Habari Kaka naomban ushauri wako, mimi nib inti wa miaka 25, sijaolewa ila nina ujauzito ambao ni wa mpenzi wangu, bado sijamuambia, ninja uhakika kuwa ni ujauzito wake lakini kwa maisha yake naona kama tutasumbuana. Huyu Kaka ananipenda sana lakini bado hana kazi, nimeanaishi kwa Dada yake na alishanitambulisha mpaka kwao.

Wakati nimeenda kujitambulisha nilikutana na mume wa dada yake, alinipenda na kunifuatilia mpaka kupata namba yangu, hapo ndipo tulianzisha mahusiano, amenitafutia kazi nayeye ndiyo kanipangishia nyumba, aliniambia kuwa anataka nimalize mtoto kwakua mke wake yeye anazaa watoto wakike tu.

Nilikubali na kubeba mimba yake ila bado sijamuambia kama nina ujauzito wake kwani najihisi kama nimefanya kitu kibaya. Mwanaume wangu yeye ananipenda, anajua kuwa hii nyumba nimepangishiwa na wazazi wangu na anakuja hapa mara nyingi kulala, ananiambia kuwa anataka tuanza kuishi pamoja lakini mimi sipo tayari kwa hilo.

Shida inakuja Kaka, juzi wakati naongea na mpenzi wangu akawa anamlalamikia Dada yake, alikua anasema kuwa ametekwa sana na mume wake kiasi kwamba Biashara zote anasimamia mwanaume wakati ni malaya. Analalamika kuwa dad ayake hamjali na ndiyo sababu ya yeye kutaka kuja kuishi na mimi kwani anaona kama anapoteza muda.

Nilipomuuliza vizuri ndipo aliniambia kuwa, Biashara zote ni za dada yake na huyo shemeji yake ni kama kachukuliwa tu kuishi naye, hawana hata ndoa na hamiliki chochote ila dada yake anamuamini kuliko ndugu zake. Yaani Kaka kumbe hata watoto wa dada yake si wa huyu mwanaume, ni kwamba yeye ni chawa tu kwa dada yake anasimamia kila kitu.

Sasa kaka nisaidie, nawaza nikimuambia huyu mwanaume nina mimba yake ataweza kuhudumia wakati naye analelewa. Vipi dada yake akijua tukafukuzwa wote nitaenda wapi? natamani nimuambia huyu mpenzi wangu kuwa nina mimba yake lakini nahofia je sjhemeji yake hataleta shida, nisaidie Kaka maana nahisi kuchanganyikiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top