NJIAPANDA; AMEMUOA MDOGO WANGU LAKINI BADO ANANILAZIMISHA KUFANYA NAYE MAPENZI

0

Tulikua tunapendana, yeye ndiyo alikua kila kitu kwangu, kama ungemuuliza mtu mwingine yoyote angekuambia kuwa ni mume wangu. Nilikua nikimuamini kuliko kitu kingine chochote kile. Lakini mwaka jana kila kitu kilibadilika, sijui hata mambo yalianzaje lakini alikua anajiandaa kuja kwetu kila kitu kilishakamilika.

Wakati huo yeye alikua akiishi Dar na mimi nilikua nimehamishiwa Dodoma makao makuu, kwakua tulikua tukiishi pamoja kabla ya uhamisho nilikua sijahamisha baadhai ya vitu vyangu. Ilikua niende Morogoro nyumbani ili kuweka mambo sawa kabla ya yeye kuja nyumbani.

Nikliwa njiani nilikumbuka kuwa nina vitu vyangu vingi vipo dar, nikampigia simu kumuambia kuwa nakuja dar lakini hakupokea, simu iliita zaidi ya mara tano hakupokea. Moja kwa moja nilijua labda yuko bize na kazi, nikakanyaga zangu mafuta huyo mpaka nyumbani kwake ambapo palikua ni kama kwetu.

Nilipaki gari na kuingia kufungua mlango, ile nafungua mlango naingia chumbani namkuta kalala na mdogo wangu, ndiyo, mdogo wangu mtoto wa Mama yangu mdogo. Nilihisi kuchanganyikiwa, baada ya kuniona badala ya kuniomba msamaha alianza kunitukana akiniambia kwanini simuamini nimeenda kumfumania, alinitukana sana na kuniambia nichukue vitu vyangu niondoke.

Wakati huo mdogo wangu alikua akicheka tu huku akimuambia kuwa hanitaki hapo, niondoke au aondoke yeye huku mwanaume wangu akimbembeleza sana kuwa asiondoke. Kwa aibu nilichukua mabegi yangu, nikapakia kwenye gari kisha nikaondoka zangu, sikurudi Morogoro, nilienda hotelini nikiamini kuwa atanitafuta kuniomba msamaha lakini haikua hivyo.

Nilikaa dar kwa wiki nzima, kila nikijaribu kumpigia simu hapokei, kila nikituma meseji hajibu. Mwisho niliamua kumtafuta rafiki yake ambaye alikua ni kama Kaka yake, nilimuambia kila kitu kilichotokea lakini naye hakutaka kuongea na mimi, alikua kama ananikwepa. Ingawa niliamua kuwa sitaki kushirikisha familia lakini baada ya kuona mambo yanakua mabaya niliamua kufanya hivyo.

Nilimpigia mdogo wake wakike ambaye mimi ndiyo nilimtafutia kazi nzuri, alikua ni kama shoga yangu, nikamuuliza kuhusu Kaka yake lakini naye ni kama alisita, alinizungusha sana lakini mwisho aliniambia “Sadiki kaenda kujitambulisha na kutoa mahari kwa mwanamke wake, nadhani utakua unamjua, aliniambia huku akinitumia na picha. Hazikua nyingine bali ni picha za mdogo wangu, alikua kanizunguka na kwenda kumtambulisha mpenzi wangu kwao.

Iliniuma sana, nililia sana, nikalazimika kuwaambia nyumbani kuwa nimeahirisha lakini baadhi ya ndugu walikuwa wakimfahamu huyo mwanaume hivyo walishajua kuwa kaniacha na kumpeleka mdogo wangu kumtambulisha. Basi nilirudi zangu Dodoma, kazini kila mtu alikua anajua kuwa naenda kumtambulisha Sadiki, ilikua shida kwangu kuwaambia kuwa nimeahirisha, nilitoa sababu nyingi lakini nadhani watu walishaambiana hivyo kuishia kunionea huruma mimi.

Nilihangaika sana, niliumia na kujaribu kumsahau lakini vijembe vya ndugu zangu, Mama yangu mdogo kila siku alikua akinipigia simu kunitukana kuwa nataka kuharibu ndoa ya mtoto wake. Mimi nilikua sijamtafuta na nilishaamua kuwa sihangaiki naye, lakini bado walikua wanagombana na nilisingiziwa mimi, niliumia sana kwani hata Mama yangu mzazi siku moja alinipigia simu na kuniambia kama mwanaume kaamua kuniacha basi nimuache niache kujidhalilisha kwake.

Niliumia kwakua sikufanya hivyo lakini sikua na namna, miezi mitatu baadaye, nikiwa nimeshaanza kupona mwanaume alinitafuta, nilishamblock katika kila namba hivyo alitumia namba nyingine. Niliposikia sauti yake nilikata simu lakini alinitumia meseji akiniambia “Huwezi kuniacha kirahisi namna hiyo, nimepoteza muda mwingi kwako inabidi unisamehe tu.”

Niliishia kucheka nikiamini kuwa ananikumbuka labda bado ananipenda. Kwa dharau nilimjibu meseji yake kuwa simtaki lakini alisisizia tuonane, nilimuambia hapana ila akaniambia kuwa yeye haachwi kizembe namna hiyo hivyo niingie Whatsapp. Niliingia ndipo nilikutana na picha zangu za uchi ambazo nilikua nikimtumia nikiamini kuwa ni mume wangu hawezi kunifanya chochote.

Zilikua nyingi za ajabu ajabu ambazo tulikua tunatumiana, sijui kwanini hakuzifuta kwani simu yake nilikua nashika na nilikua sijawahi kuziona, mara nyingi tukitumiana picha huwa tunaambiana futa, mimi nafuta kumbe mwenzangua alikua hafuti. Hakuandika kitu chochote lakini nilijua alichokua akimaanisha, aliniomba kuonana na mimi kwangu, alikuja na kuniambia wazi kuwa hawezi kuniacha.

Alifanya makosa kujitambulisha kwa mdogo wangu zilikua hasira ila ananipenda na hawezi kuniacha. Tulifanya mapenzi siku hiyo, ni kama alinibaka kwani aliniambia wazi kama sitakubali atasambaza picha zangu. Hali hiyo iliendelea hata alipomuoa mdogo wangu mwaka huu mwezi wa pili. Yaani pamoja na kuniambia kuwa hampendi ananipenda mimi lakini kamuoa na wanaishi pamoja.

Sababu ya kuja kwako ni hivi, X wangu kaoa lakini kashanifanya kuwa mtumwa wake wa ngono. Anakuja kwangu anavyojisikia, yaani kila akiwa Dodoma ni lazima kuja kwangu na anataka kufanya mapenzi, nikimkatalia ni lazima kunitumia picha zangu za uchi akinitishia kuwa kama nikimkataa basi atazisambaza.

Ananifanyia mambo ya ajabu, ananilazimisha kufanya mapenzi kinyume na maumbile, ananilazimisha kumfanyia vitu vya ajabu, huku akiniambia kuwa ananipenda na kuendelea kunitishia kusambaza picha zangu. Nimekua mtumwa kwake, natongozwa na wanaume wengine lakini naogopa, ingawa ananiambia hata nikipata mwanaume mwingine niolewe ila hawezi kuniacha.

Ananiambia kuwa nikiolewa kama yeye ambavyo ameoa na kuchepuka na mimi basi nitakua mchepuko wake la sivyo ataniaibisha. Nahisi kuchanganyikiwa nikiwaza haya mambo, sijui nifanye nini kwani maisha yangu yamesimama, nahisi kufa, kuna wakati natamani hata kunywa sumu kwani nimechanganyikiwa.

Nahisi siku akivujisha picha zangu hata kazi naweza kupoteza, vipi kuhusu Baba yangu si atakufa kwa presha, nimechanganyikiwa sijui chakufanya nisaidieni nifanye nini ili kuondokana na hii hali kwani nimechoka sana. Anaweza asikutafute wiki lakini akakutumia kavideo kako kisha akakuambia usikae kimya hivyo utanikasirisha, yaani nashindwa kujua nifanye nini?

MWISHO

Credit IDD Makengo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top