SWALI; Mwanaume wengu ameniambia nikipata mwanaume mwingine niolewe je huyu ananipenda?
JIBU; Hili ni swali ambalo linawachanganya wanawake wengi, Kuna sababu mbili za mwanaume kusema hivi, soma kwa makini kujua kama anakupenda au la?
(1) Unalalamika sana kuhusu ndoa wakati yeye hajawa tayari hasa kimaisha; Mko kwanye mahusiano, labda ni ya muda mrefu au mfupi, ameshakuambia mara nyingi kuwa yeye bado hajawa tayari kuingia kwenye ndoa, lakini kila siku unalalamika, utanioa lini, lini unakuja kwetu, nimechoka, mbona huonekani siriasi.
Wakati mwingine humuulizi moja kwa moja bali ni kwa kuzunguka kama; mimi umri wangu umeenda, nataka nikifikisha miaka flani nina mtoto, rafiki zangu wote wameolewa, natamani ndoa yangu iwe hivi, nyumbani wananisumbua.
Kama ni mtu wa kulalamika kwa mwanaume akikuambia “Ukipata mwanaume mwingine olewa.” Huyu mara nyingi ni mwanaume anayekupenda lakini kwakua umezidisha kelele basi anaamua kukuambia kwa hasira, unamsumbua na kashachoka hivyo kama unampenda kweli usitafute mwanaume mwingine na mpe muda kwani unamkatisha tamaa.
(2) Humsumbui mara kwa mara kuhusu Ndoa; Hapa, kama si mtu wa kuongea kila siku, labda mlishaliongelea mara moja tu au hata hamjawahi kuongelea na si kitu ambacho kipo kwenye mipango yako ila ghafla anakuambia hivyo basi jua kuwa huyu hana mpango na wewe.
Ameona umekua mwema kwake na yeye hana mpango wa kukuoa, hataki kukuumiza au hataki huko mbeleni uje kulalamika kuwa alikupotezea muda wako. hapa kubaliana na ukweli na muambie huwezi kuwa naye huku ukitafuta mtu mwingine.
Anza maisha yako, kama atakubali umuache basi jua kuwa alishakuacha muda mrefu ila alikua akikutafutia sababu.
(3) Haamini kama unampenda anakutega; Kuna baadhi ya wanaume hawajiamini, haamini kuwa unampenda, huyu anaweza kukuambia hivi ili kukupima kama unampenda kweli au unaweza kumuacha. Mara nyingi mwanaume kama huyu utajua tu, kwanza anaonyesha upendo sana, wanakua na wivu sana, ana wasiwasi sana na mara nyingi anakua mtu wa kuogopa kama utamuacha, unaona anataka kukuoa lakini kipato chake hakijakaa sawa hivyo ni kama anapima kama utamvumilia au la. Huyu kama unampenda muambie siwezi tafuta mwingine nakusubiria wewe.