SABABU 3 KWANINI USIMTUMIE MPENZI WAKO PICHA ZAKO ZA CHIU!.

0


Wanawake wakipenda wanaamini sana, wanakua tayari kufanya kitu chochote kwaajili ya wanaume. Wanawake wana shida moja, hawajifunzi kabisa, mwanamke akishapenda akili yake inakua haifanyi kazi anaamini kua hakuna kuachana. Yaani hata kama huko nyuma alishakua na mwanaume akaumizwa.

Lakini bado akikutana na mwanaume mwingine basi anachanganyikiwa na kusahau kila kitu. Anamuamini kwa kila kitu, najua unasema ni mume wako, unasema ni mpenzi wako, unamuona mstaarabu lakini kamwe! Kamwe! Kamwe kama auna akili usitume picha za uchi kwa Mwanaume na hizi ndiyo sababu kuu tatu.

(1) Watu wanaachana na kwakua wanaume hawafuti picha za uchi basi ni rahisi mwanaume kutumia picha zako kukudhalilisha. Najua unasema huyu wa kwangu ni mstaarabu lakini muulize X wake, waliachana kwa sababu gani, muulize kama ni mstaarabu au la, dada yangu labda kama yeye badala ya masikio ana pembe ndiyo tofauti!

(2) Ana mchepuko wake mmoja au rafiki yake mmoja wakike ambaye anawaonea wivu na ana password yake, hata yeye anaweza aisjue lakini yupo mtu anaijua, hajaamua tu kuitumia na mara nyingi mchepuko na rafiki wakike wana wivu sana, siku akiishika basi utaisoma namba. Sasa labda kama wewe una uhakika asilimia 100 kuwa hachepuki na hana marafiki ndiyo tuma tu.

(3) Simu zinapotea na picha zikisambaa anakuacha kwakua wanawake ndiyo huaibika. Dada labda kama umeongea na Mungu kuwa simu yake haitapotea, wanaume hawafuti hizo picha, atakuambia amefuta na wewe kukagua simu yake ila siku simu ikipotea ikaokotwa na mtaalamu au siku mkikorofishana ndiyo utajua hujui.

Nimalizie kwa kusema hivii, achana na haya mambo, narudia kama anakuambia kuwa anataka kuhamasishwa ongea naye lakini video call uchi, kupiga picha uchi eti ili asichepuke, Dada huna jipya na wala huna maajabu. Kama ni wakuchepuka atachepuka tu, najua mnahisi mnahamasisha lakini hakuna kitu mnajidhalilisha tu!.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top