Sijui tuwaambie ukweli au tusubiri mpaka wakishabeba na Mimba zao!

0Tatizo dada zangu unatembea na mume wa mtu lakini hata kudanga hujui, sitakiwi niwaoneee huruma ila unatembea na mume wa mtu, anakununulia kiwanja, yaani yeye anatoa pesa yake mfukoni, anaenda kwa Mwenyejikiti, analipa yeye anakununulia kwanja. 

Anakufungulia duka kaandika jina lako halafu anakupa wewe, anakuopangishia nyumba anakununulia kila kitu, kodi ambayo huwezi kulipa hata uuze na ndugu zako anakulipia, halafu eti unategemea mwanaume wa namna hiyo siku umepata mwanaume wako ambaye hata ukimuambia atume na ya kutolea ana screenshot na kupost kwenye group unamuambia naolewa, akuache hivi hihivi?

Kuna vitu mwanaume akikupa jua kuwa anakununua, hata ukiolewa basi utaendelea kutumikia Club tu unakua huna namna maana hata kama asipokunyang’anya ila atakusumbua sana kudai hivyo vitu.

Angalau basi tuseme mwanaume mwenyewe ana pesa ya kueleweka, kwamba yeye kukujengea nyumba ni sawa na Mchaga kukutoa out kukununulia Savanna ukalewa, lakini pesa zake naye za manati, ana mikopo mingi! Mwanaume yupo KIKOBA ana marejesho, ukute sasa Mpare anakuhonga nyumba useme eti nitamuacha hivihivi Dada yangu si kwa maisha haya.

Natamani hata niwaambie cha kufanya ila achene kudanga, watu watulie na ndoa zao!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top