UNAKUBALIANA KUWA MWENZA SAHIHI UTAMPATA KANISANI/MSIKITINI? NA SIO KWINGINE

0

Bila shaka hata wewe utakuwa unajiuliza kama ni mwanaume utakuwa unajiuliza nani mkweli watumishi wa Mungu wanaosema wake wanaofaa kwa ndoa watapatikana katika madhabahu hayo au wanasaikolojia na mitazamo ya kijamii ambayo inaamini mke unawezaa kumpata popote! hapo nani ni mkweli.
Nilimuuliza mtumishi mmoja wa Mungu akanambia kuwa 'Mwanamke wa Kuoa atapatikana katika madhabau,iwe kanisani au msikitini,hivyo wanaume kama unataka mke mwema basi utampata huko' je kwa kauli hii wewe unakaubaliana nayo kwa asilimia ngapi?
JE! MWANAUME ANAHITAJI MKE WA AINA GANI!.
Niwambie kuwa wanaume kila mmoja anavipaumbele vyake sio wote watahitaji kama mwingine anavyohitaji,kuna mwanaume anahitaji mwanamke msomi!,mwingine anamhitaji sex ambaye atamridhisha kwenye mapenzi bila kujali watapata mtoto au la! atapenda mwanamke huyo awe vile vile siku zote,
Kuna mwanaume anahitaji mwanamke wa Kumtawala,atakaye kuwa kama mtumwa akisema kulala anaenda kulala,akisema usisuke hasuki,akisema utakaa hapa nyumbani atakaa,wanaume hao wapo wanahitaji wanawake watakao kuwa watumwa katika ndoa kwa furaha ya Mwanaume.
Lakini Kuna wanaume wanaohitaji Mke wa Kujishughulisha,mwenye kupambana bila kujali hiyo kazi inamwingizia shilingi ngapi kikubwa anasaidia familia au anaweza kusimamia shughuli zake za Miradi n.k
#Kifupi tambua kuwa Kila Mwanaume anamahitaji yake ya tofauti,kuna mahitaji ya Jumla na mahitaji yasiyo ya Jumla ya mmoja mmoja na hayo mara nyingi ndio hupelekea mtu kuoa mwanamke sahihi au asiye sahihi!.
'Siku Nyingine tutazungumza juu ya wazazi kushiriki kukuchagulia mchumba leo tukamilishe hili kwanza'
JE! MIMI NAAMINI NINI KUHUSU WAPI UTAMPATA MTU SAHIHI KATIKA NDOA.
Mimi ni muungwana wa kuamini kile kinachonisaidia katika maisha haijalishi utampata Mbele ya kanisa,msikiti,katika chombo cha moto au bar n.k kikubwa je anakidhi mahitaji yako? je atakuwa sehemu ya furaha ukiwa nae kwenye ndoa,je! mtashikamana bega kwa bega,Je umefikilia akiwa mzee utaendelea kumpenda vile atakavyokuwa? na hii imekuwa changamoto wengi wetu hili hatuangalii kesho ya uzee wenu unaangalia kwa sasa.
Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa akikutana na mwanamke siku moja akimridhisha katika ngono kesho anamuomba amuoe sababu amemridhisha usiku huu mmoja je! inatosha ngono kutumika kupima? lah hasha.

KUHUSU VIONGOZI WA DINI.
Naomba nieleweke siwapingi kwa lolote ila tutambue kuwa sisi wote ni wa Mungu,ndio maana mnapokea watu waliooana huko wakija kujiunga nanyi kumtumikia Mungu hamvunji ndoa zile,mnachofanya ni kuikabidhi kwa Mungu,hivyo ingekuwa ni kwamba watapatikana hapo ningeelewa kama mngekuwa mnazivunja kisha mseme sasa utampa aliye wako ukiwa hapa. 
Kwenye hili tutoke na moja kuwa mchumba unaweza mpata popote kikubwa atakidhi mahitaji yako!,sababu wewe ndie utakaye ishi nae katika maisha yako wala sio mchungaji,wala si mimi wala si wazazi wako!.
Ni nayo mengi ya kukueleza kuhusu hili somo lakini wengi wetu wavivu kusoma hebu leo tuishie hapa kesho tutachambua zaidi.
Nawaombea nyote ambao hamjapata mwenza mwema Mwenye Mungu awajalie Mpate na muishi kwa amani na Upendo
usisahau kutembelea kurasa zetu za facebook page. www.facebook.com/idawamedia / tamtam ya Penzi

share like & comment hapo chini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)
Youtube Channel Image
Henrick Idawa Subscribe To watch How to Earn Money

 

 
#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top