UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UNAVYOCHANGIA WANAUME KUPIGA WAKE ZAO!

0

Najua wanaume wengi wanaogopa kukiongelea hiki kitu kabisa, wanaona kama ni aibu na wakati mwingine wanalazimika kudanganya ili tu nao kuonekana kama wanaume shupavu. Nadhani tatizo linaanzia hapa, wanaume wangi wanaishi wakidhani kuwa wana matatizo hivyo kujikuta kila siku wanakua na visirani, kujikuta wanalazimika kuwa Malaya, wanalazimika kuwanyanyasa wanawake zao kwakua wanajiona wao si wanaume kamili na wanadharaulika.

Ukisikiliza kesi nyingi za wanawake wanaolalamika kupigwa, wanaolalamika kunyanyaswa, wanaolalamika wanaome zao kuchepuka tena kwa dharau utakuta wanaume wao wana sidfa kuu moja. Katika kufanya tendo la ndoa wanaenda raundi moja na hata wakienda mbili basi ni kwa shida, lakini hiyo raundi moja mara nyingi haivuki dakika kumi. Ni wengi, ni wengi balaa ambao wanaume zao wanawanyanyasa na ukiangalia wana hii sifa.

Hii inatokana na ukweli kuwa, jamii imekua ikiwaaminisha wanaume kuwa, ili uonekane una nguvu za kiume lazima uende raundi tatu na kuendelea na zichukue dakika angalau 30 na kuendelea. Hivyo mwanaueme wa raundi moja ya dakika tano anakua hana furaha, hana amani na anajiona kama kasichana ambako hata bado hakajavuja ungo. Anajidharau na kibaya zaidi anadhani kuwa kila mtu anamdharau, kwamba mwanamke wake anamdharau, mwanamke wake haridhiki, mwanamke wake anachepuka.

Hii si kweli, katika tendo la ndoa, kumridhisha mwanamke hakuna uhusiano na dakika au idadi ya magoli. Kuna watu wanaenda masaa mawili lakini hakuna wanachofanya zaidi ya kuwaumiza dada za watu na kupakana mijasho tu. Lakini kuna watu wanaenda dakika tano ila mwanamke akitoka hapo anawehuka kabisa, yaani utamu anaopata mpaka hatamani kuchepuka.

 Kwa maana hiyo mwanaume, muandae vizuri mpenzi wako, kiakili katika maisha ya kawaida na kitandani, ingia uwanjani vizuri acha kujipa presha ya kwenda dakika 30 furahia hizohizo tano, dakika tano si ugonjwa, acha kujichukulia kama umekufa kama si mwanaume vile!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top