USIMLAUMU ALIYE KUTUMIA KINGONO/KUKUCHEZEA TU NA KUKUACHA, BALI JILAUMU KWA KUKUBALI KUTUMIWA

0Amosi 3:3
" Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?"

Wagalatia 6:7
"Msidanganyike, Mungu HADHIHAKIWI; kwa kuwa cho chote APANDACHO mtu, ndicho ATAKACHOVUNA"

Mara nyingi unaweza kuwasikiliza mabinti/wanawake wakilalamika juu ya wanaume kukosa uaminifu mara baada ya kuwa wameshiriki NGONO, na kuwaona wanaume ndio watu wa ovyo kabisa.

Hii hutokana na sababu zisizo pingika kuwa mwanamke huwa mwathirika zaidi kuliko mwanaume pale wanapoacha ikiwa walikuwa wamekwisha KUJAMIANA. Saikolojia ya mwanamke hufikiria kuwa jamiii yote inatambua amejamiana na mtu fulani, lakini amemwacha(Malaya/muhuni). Dhana hii huwaumiza wanawake wengi mno.

KUJAMIANA kamwe hakuwezi kufanyika na mtu mmoja tu, ukifanyika kwa mtu mmoja tu hapo ni kujichua/Punyeto ambapo tendo hili hufanywa na mtu mmoja kuiridhisha nafsi yake either kwa Sabuni, Mafuta, kifaa chocho chenye umbo la Uume(Test tube, Tango/ndizi). Hili ni tendo linamhusu mtu mmoja na nafsi yake.

Kukosekana kwa mbegu ya Utulivu/uaminifu/Kujiamini/Uvumilivu kwa Mungu kwa baadhi ya Wanawake/mabinti kumepelekea kupoteza dira ya msimamo ulio MADHUBUTI mbele za Mungu na kuwaamini WANAUME waliojenga nao mahusiano na kupokea kila wanachoeleza kwa kudhania ndio Upendo, kumbe upendo sio kwa KUJAMIANA tu.

Inatokea mahusiano yamekuwa kwa muda fulani, na kwa sababu katika hatua za awali za mahusiano kabla ya Ndoa kunajengeka tabia ya kuitana majina ya kila namna Mara Mke/Mume wangu mzuri, Baby, Honey, My Everything, My King/Queen n.k inaifanya akili ijihalalishie kuwa kweli huyu ni Mali yangu hata Kama hamjaoana.

Ikiisha fikia hatua hiyo, lolote analoweza kusema Mwanaume unakuwa radhi kufanya maana unaamini ndie Mume, maana imezoeleka mwanaume ndie mchokozi/mwanzishi katika kuhitaji KUJAMIANA. Moyoni mwa mwanamke hufikiria kuwa kwa nini nimbanie mume wangu, ngoja nimpe tu maana hata nikimbania Leo kesho nitampa maana ndie Mume, bila kujua kilichopo nyuma ya huyo mwanaume.

Mwanamke ndie mwamzi wa mwisho, Either NGONO ifanyike au isifanyike. Kwa kuwa mwanamke ndio mwenye uamzi, Basi mahali Popote palipo na utengano baada ya KUJAMIANA mwanamke anakuwa amevuna alichopanda.

Kama mwanamke angelikataa kwa kujiamini ni dhahiri kuwa neno la kusema kuwa wanaume ni wahuni baada ya kuvuliwa nguo, ilipaswa mwanamke atambue kuwa yeye ndie mhuni aliyekubali ngono iwe juu ya mwili wake.

Wote wawili mbele za Mungu ni watenda DHAMBI, na tabia ya dhambi huondoa Utukufu wa Mungu kwa mtu. Hivyo ukiona baada ya KUJAMIANA Mambo yanaenda kombo Tambua Utukufu wa Bwana haupo nawe maana umeharibu yote mazuri uliyokuwa umekusudia.

Yeremia 5:25
"MAOVU yenu yameyageuza haya, na DHAMBI zenu zimewazuilia MEMA msiyapate."

Usiwe mtumwa wa Dhambi, na kumsingizia mtu kuwa yeye ndie sababu ya Maisha unayoishi. Tambua nafasi ya Mungu katika Maisha yako ili uwe huru.

Yohana 8:32
 "Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.

SIKIZA HII KWA KUBOFYA PLAY au DOWNLOADPost a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top