W A R A K A K W A W A N A U M E .

0

Kuna baadhi ya wanaume katika hali ya kuwa-please wanawake zao wanaowapenda wamejikuta katika hali mbaya. Wameumizwa na mahusiano, wamefilisika na kupoteza muda wao wa kutosha. 

Kuna idadi kubwa ya wanaume ambao wanamaumivu makali mioyoni mwao ila wanaugulia maumivu hayo kimya kimya. Ni kwa sababu mwanaume alieumizwa na mwanamke imezoeleka haitakiwi alie, haitakiwi alalamike kwa minajili kwamba ataonekana yuko 'soft' sana. 

Ila kiuhalisia wapo wanaume wengi sana mioyo yao inateketea na hali hiyo inapokua imezidi, baadhi yao hujiingiza katika ulevi kwa minajili ya kuondoa stress, wengine huanza tabia ya kubadili wanawake kwa minajili ya kulipiza kisasi na hii hupelekea kuwaumiza wanawake wengine ambao hawana hatia sababu tu yeye aliumizwa na mwanamke mmoja tu aliempenda.

Na bahati mbaya muda mwingine unakuta mwanaume anamuoa mwanamke, lakini mara tu baada ya kuingia kwenye ndoa mwanamke anabadilika tofauti na vile alimfikiria angekua. Na kwa sababu siku zote mwanaume ndio hutupiwa lawama endapo ndoa itakufa, hubaki kimya na maumivu yake pasina kuomba ushauri mahala popote pale. Zaidi huenda Bar kupunguza stress, hata wazo la kwenda kwa viongozi wa dini kwa msaada wa ushauri na sala hua halipo.

My brother, nisikilize mimi na nisikilize vizuri. Haitajalisha ni kitu gani unamfanyia mwanamke wako, kila mwanamke namna alivyo hujua ni nini anakitaka na anao uwezo wa kukipata. Unaweza ukamnunulia gari, ukampa pesa unazoweza, ukajitahidi kumuonesha mapenzi kadiri unavyoweza lakini kama ndani ya moyo wake ameamua you are not the one, atakuacha tu na kwenda kwa mvulana tu wa ajabu ambae hana chochote zaidi ya jina kubwa Instagram na anaevaa nguo za rangi rangi. Hauwezi kumlazimisha mwanamke awe muaminifu.

Mwanamke ambae anakuhitaji, huvutiwa na wewe na siku zote hua chini yako, hua haihitaji kumbusho la kila siku la kuwa muaminifu kwa sababu hilo Huja lenyewe naturally. Hua haina haja ya kum-control kwa sababu anafahamu fika kipi ni sahihi na kipi si sahihi katika mahusiano.

Mwanamke yeyote yule ambae wewe unafikiri unahitaji remote control kuhakikisha unam-control mienendo yake kila siku hakufai. Mwanamke huyo akiamua anaweza kupaki Rav4 uliyomnunulia na kwenda ku-cheat na mtu wa ajabu tu. Hapa suala sio mambo mazuri uliyomfanyia, anachojali yeye moyo wake uliko. Mwanamke kama huyu atakuacha na maswali mengi na ukajiuliza juu ya uanaume wako!

My brother, nisikilize kwa makini. Hivi unajua ni rahisi sana kumkamata kiongozi wa kundi la kigaidi la ISIS au Boko Haram, kuliko kumkamata mwanamke anaesaliti? Anaweza akakusaliti katika gari uliyomnunulia, nyumbani kwako, na akavuliwa nguo ya ndani ambayo wewe umemnunulia na usiweze kabisa kumkamata.

Hivyo basi, mwanamke anapokuonesha dalili za kuchepuka au ukamkamata anachepuka wala usishangalie kwamba umemkamata..hujamkamata, ni kwamba yeye mwenyewe ametaka ujue...ni kwamba tu anakutumia ujumbe kwamba "Sikuhitaji tena, fanya maaumuzi ya kuendelea na maisha yako sasa"

Counseling haitasaidia. Maombi yatakufanya ujisikie poa ila hayatamrudisha. Sio kwamba Mungu hajasikia kilio chako, ni kwa sababu Mungu mwenyewe anajua kwamba huyo sio sahihi kwako na endapo atarudi atakuumiza zaidi.

Kiuasilia tu wanawake huwaheshimu wanaume wanaowapenda. Anaweza akawa mchungu na mkaidi kwa wanaume wengine, lakini kwa yule ambae yeye anaempenda kweli ni kama mbwa mbele ya chatu namna alivyo mpole. Unaweza ukadhani amerogwa..lakini hapana amependa kweli na hatakua tayari kuona akikupoteza kwa namna yoyote ile.

My brother kama umepata mwanamke wa aina ya "utaniambia nini wewe? Huwezi nifanya lolote!" Men huyo hakufai. Kama ukiona anabishana na kupayuka hovyo hovyo bila heshima yoyote ile sio mara moja, bali mara nyingi na ndio tabia yake...my brother huyo sio..amua sasa na jiokoe na maumivu zaidi huko mbeleni. Mipango yake ya kuongea nae haitafanya kazi.

Na kadiri utakavyozidi kumfanya aone anachofanya sio sahihi, ndivyo atakavyozidi kukusukumia mbali. Bahati mbaya anaweza kuwa ni mke wako, lakini akaja kukutana na soul mate wake, na bahati mbaya zaidi sio wewe. 

Huna haja ya kufight kudhihirisha kuwa wewe ni mwanaume. Kama kiuhalisia tu hajaona kuwa wewe ni mwanaume licha ya jitihada ulizozionesha katika kumjali na kumpenda, my brother she is not the one. Muombe Mungu na Fanya maamuzi! 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

 

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top