WANAUME MNAO WADHARAU DADA WALIOZALIA NYUMBANI MNAHITAJI TOBA!

0

Je ulitaka atoe hiyo mimba baada ya kumtelekeza?? Tena inawezekana ulimwambia utamuowa lakini baada ya kumjaza mimba umemkimbia, kumbe lengo lako lilikuwa ni kupata NGONO tu!

Inawezekana wewe mwanaume pia mama yako alizalia nyumbani, na bado hata wewe unaonyesha dharau kwa wadada walio zalia nyumbani, je angeamua kuitoa hiyo mimba leo ungekuwepo duniani?

Sababu za kuzalia nyumbani ni nyingi, mfano kubakwa,kushawishika kutokana na mazingira magumu.

Hebu fuatilia makuzi mengi ya yatima,wazazi na walezi wa kufikia,utmikishaji watoto kingono nk. 

Bora dada akipewa mimba azae mtoto wake na amlee kuliko kutoa hiyo mimba ili tu asubiri kuolewa tena. 

Bahati mbaya anaweza akatoa mimba asiolewe na mtoto asipate tena maishani. Hawa ni mama zenu muwaheshimu.

Acheni kuchuma laana bure kujifanya wema na watakatifu wakati usiku na vichochoroni mnawabaka hadi wanawake vichaa na kuwapa mimba.

Wanazaa katika mazingira magumu na hatari,wanalea kwa taabu na kwenye makuzi hatarishi halafu mtu na akili,heshima na utu wako unadiriki kuwasimanga eti siwezi kuoa au kumheshimu mwanamke aliyezalia/zalishwa nyumbani?

Wakati mwingine maisha yetu yanakuwa magumu na misukosuko sio kwamba hatuna akili,nguvu au uvivu wa kufanya kazi kwa bidii!!

Laah! Tumejikwaa kwenye makosa kama haya na kuumiza wengine na kujeruhi mioyo yao,kadri wanavyoteseka na viumbe wasio hatia mliowatelekeza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top