WANAUME WASHAURIWA KUWAZUIA WAKE ZAO KWENDA KWAO KUOKOA NDOA ZAO.

0
KUNA WAKATI INABIDI UMKATAZE MKE WAKO wako kwenda nyumbani kwao Mara kwa mara ili kuokoa ndoa yako, hata kama mnaishi mtaa mmoja, lakini tabia ya mwanamke kila siku kwenda kwao inaua ndoa nyingi sana na ni sababu ya kufanya wanaume wengi kuwa mazezeta! Najua mnashangaa, na kuna baadhi ya wadada watatoa mapovu lakini ndiyo ukweli! Ukishaolewa unapaswa kujua kuwa unaenda kuanza familia yako, ndugu zako wanabakia kuwa ndugu lakini mume wako uanakua mshirika wako na familia yako.

Kila siku mwanamke unaongea na Mama yako, lakini kila wiki unataka kwenda kumsalimia! Umeshaolewa lakini badala ya kuanza kuwa mke, kuwa Mama unaanza ushoga na Mama yako, mnaongea nini kila wiki unachoenda kuongea naye, kuna nini cha maana ambacho kwenye simu hakiishi! Kitu cha kwanza kabisa mwanamke unachotakiwa kujua nikuwa Mama yako ni mzazi wako, acha kumfanya shoga yako kumuambia kila kitu kinachotokea kwenye ndoa yako.

Nilazima kuwa na akili ya kupima, kujua kipi nimuambie Mama na kipi nikae nacho. Unajikuta unaongea na Mama yako kila siku mnakosa hata chakuongea mpaka mnaanza kujadili hata mume wako anaenda round ngapi, mnaanza kujadili kibamia cha mume wako na Mama yako! Ongea na Mama yako kila siku kwenye simu sawa, akimwa nenda kamsalimie hata kama ni kila siku, lakini kama ni mzima, angalau kaa miezi miwili nenda mara moja na hiyo ni kama mko karibu, si kwakua mko karibu kila wiki uanenda, yaani unakua kama unaishi kwenu.

Tena kama kwenu mna kauwezo kiddogo ndiyo kabisaaa, mwanaume wa watu hapumui! Mara ooo Mama kaniita, tena huombi hata ruhusa unampa tu mwanaume taarifa kwamba nipo kwa Mama. Wanawake wengine ni mizogo kabisa, unakuta anaenda na watoto kwa Mama yake, anapikia huko huko mume anamletea kwenye Hotpot, huo ni upuuzi kabisa.

Mama yupo mkoani lakini humalizi mwezi unataka kwenda, nimemmiss Mama. Mwanaume kama una mwanamke wa namna hiyo basi huna haja ya kuongea mara tatu, ukishamuambia kua sitaki tabia hii basi muangalie, akirudia tena muambie, mara ya tatu unaona kila kitu ni Mama tena anakubania na pua kabisa “Siwezi kuishi bila Mama yangu.” Huna haja ya kuongea, akienda wewe tafuta Kiruikuu, pakia vitu vyake mfuate nyumba, mpelekee na muambie “Mkimalizana na Mama yako utarudi!” halafu ondoka zako, utakuja kunishukuru baadaye.

Dada zangu kama mnaona sauti haitoshi nyie semeni tu, kmaa umeolewa hembu usisahau ku #SHARE mume wakoa aweze kuona; NOTE; Kama umejifunza kitu hapo basi #SHARE aweze kuona;

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top