WANAWAKE WAZUIWA KUWASILIANA NA MA X WAO; WAUME WARUHUSIWA.

0

Leo tujadili hili jambo Pamoja👇👇👇👇👇
SWALI; Hivi kwanini mara nyingi unaongea kuhusu wanawake kuwasiliana na ma X wao lakini huzungumzii wanaume?

JIBU; Nikwakua mara nyingi, mwanamke akimtafuta X wake ambaye hawafanyi naye kazi pamoja, hawana mtoto pamoja lakini bado anamtafuta na ukimuambia asihangaike naye bado anahangaika naye, mwingine ukute kaolewa lakini bado anahangaika na X wake.

Mara nyingi huyo mwanamke anakua bado anampenda X wake na kama X akijirudisha asipopita naye basi anaweza hata kumuambia muache mume wako na akamuacha kweli, mara nyingi mwanamke anahangaika na X wake kwakua bado anampenda.

SWALI; Wanaume vipi mbona wao ndiyo wanaongoza kuwasiliana na ma X wao.

JIBU; Mara nyingi mwanaume akiwasiliana na X wake ni kwakua ni Malaya au kwakua hata hajali na haoni kama ni shida. Iko hivi, wanaume hawana kinyaa, hawafanyi mapenzi kwa moyo bali kwa mwili. Akimtafuta X wake na kumuambia bado nakupenda, siwezi kukuacha, sijui ujinga gani gani basi jua kuwa anataka apite naye amuache, si kwakua bado anampenda, hata hajamkumbuka, wala hana mpango naye.

Tena wengine anakutafuta akiwa na shida, yaani anaenda sehemu kikazi hana mwanamke wa kulala naye au sehemu ya kushukia anakumbuka nina X wangu flani anaomba msamaha analia kabisa, akishamaliza shida zake basi anaachana naye.

Wakati mwingine anawasiliana naye, hata hana mpango naye kwakua kazoea stori naye tu, ila mwanamke yeye anapenda na moyo hivyo mazoea kidogo sio kama anachepuka tu bali anaweza hata kuvunja ndoa yake kwa X ambaye anamdanganya.
Usisahau kuacha maoni yako hapo chini au katika kurasa zetu za mitandao facebook @idawamedia. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top