WANAWAKE WENGI WANAOLEWA ILI WAKATUNZWE ILA SIO KWA KUSUDI LA MUNGU,JE UNAKUBALIANA NA HILO?

0
Kijana ambaye unataka Kuoa au Kuolewa omba Mungu akupe MTU SAHIHI ambaye mtatembea naye katika Njia moja na siyo kufuata mali au Pesa. 

Usiingie katika Ndoa kwa tamaa au kwa sababu unataka kitu fulani la!, Ndoa ni ya Muhimu sana na ni Mali ya Mungu acheni kudanganyana.

Siku hizi watu wengi wanaoa na kuolewa na watu kwa tamaa ndio maana talaka zimekuwa nyingi sana. Oa au Olewa na mtu ambaye UNAMPENDA na Yeye ANAKUPENDA ili hata kama itatokea dhoruba ya aina gani katika Maisha yenu muweze kusimama pamoja. 

.USIOLEWE ILI UKATUNZWE:

usiolewe ila aje mtu akusaidie kimya sababu maisha ni magumu..
Sema wadada mnachagua sana ndio inasababisha chelewa olewe tangu uzaliwe yaweza umetongozwa na wanaume labda 100 jamani kweli kati ya hao Munngu akumleta mume kweli au ndio alikuja mfupi mwenye kitambi wewe unataka warefu utaki mume unataka warefu

Usiolewe na mwanaume kwa kuwa una mimba yake.
Usiolewe na mwanaume kisa anakufurahisha.
Usiolewe na mwanaume kwa sababu huna ajira.
Usiolewe na mwanaume kwa sababu umekua nae ktk uhusiano kwa muda mrefu.
Usiolewe na mwanaume kwa sababu umejiwekeza kwake kiuchumi.
OLEWA nae kwa sababu umemchunguza kwa makini na umejiaminisha kwamba anafaa kuwe mume bora na baba bora wa watoto wako.

Usijione kwa sababu  Wewe ni Mtoto wa Kike ndio unastahili kuwa  pangu pa Kavu, ACHA UJINGA. Usifanye KUOLEWA ndio SULUHISHO la Matatizo yako, ndio SULUHISHO la UCHUMI wako. 

Kuna mabinti sijui ni Uchovu au kukata tamaa, utawakuta wanalia na kuomba “Bwana YESU nipe mume nataka kuolewa,  anachana Nywele kwa Mtindo mbalimbali ili Vijana wamuone, huo ni UJINGA.
 
USIOLEWE ili UKATUNZWE, OLEWA ili  Kutimiza MAKUSUDI YA MUNGU, HUOLEWI ili Mtu AKUTUNZE, Unaolewa kwa sababu unataka kutimiza RATIBA YA MUNGU, Sio  Unaolewa kwa sababu unaona pale Nyumbani WAMEKUCHOKA au maisha ni magumu, HAPANA. 

OLEWA kwa sababu UNATIMIZA Makusudi na Ratiba ya MUNGU kwani Yeye  amesema si vema mtu awe peke yake.

Mwengine ameolewa miaka mitano hana ombi lolote kwa Mungu yeye kuomba tu matatizo ya mume wake utasikia Mungu mbadilishe mume wangu Mungu mume wangu...usiolewe na mtu akasababisha ukashindwa Muomba Mungu mambo mengine yeye akawa ndio ombi miaka yote ya maisha yako maana kila siku tatizo yeye tu kila siku maombi juu yake likiisha ombi ili linakuja jingine 

Mwalimu wako Bemasha nakusisitiza binti yangu haya yote yanatokana na uchaguzi wa mwanaume sio sahihi na kufuga changamoto kipindi cha uchumba unaona mwanaume kituko unavumilia sasa Mungu akuoneshe nini ashakuonesha huyu afai unakomaa nae tu badae unaanza kusema Mungu wangu uko wapi kwenye ndoa wakati mpo kwenye uchumba Mungu alikuonesha moyoni mwako kabisa huyu kuwa nae makini wewe ukakomaa tu unajifanya bingwa wa kuvumilia vioja na kujifanya ntambadilisha kazi ya kubadilisha mtu ni ya Mungu tu kwa manufaa ya kazi zake na sio yako kwa manufaa yako binafsi..

Binti yangu kawe na ufahamu mkubwa sana kuhusu dunia maana imeoza

Ujumbe huu umeandikwa na Mwalimu Bemasha Mungu ambariki kwa kutuelimisha Leo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top