Kuna kile kitu ambacho umezoea kumuambia mume wako kuwa akiache, hutaki akifanye, labda ni Mwanamke ambaye ni Rafiki yake, anapenda sana kuongea naye, anapenda kuchart naye, huyo Dada naye akikuona anajilegeza kwa kujifanya kama anapendwa zaidi.
Sasa mara nyingi umemuambia mume wako kuwa hutaki awe karibu na huyo mtu, umemuambia kuwa hutaki kumsikia. Ukikutana naye unanuna na ukiona hata simu yake basi unagombana na mume wako mpaka basi!
Nikuambie kitu dada, hiyo si suluhu, hakuna mwanaume atabadilika kwa wewe kumnunia au kumtishia kumuacha kama ataendelea naye, hapana, ukiacha kumpa umuhimu huyo mwanamke basi jua kuwa hata mume wako naye hatampa umuhimu. Mpuuze huyo mwanamke.
Mwanamke wa namna hiyo ni kama TOPE, ukiwa barabarani ukikutana na matope hupambani nayo kwa kuyakanyaga kwani yatakuchafua. Lakini kama ukiyakwepa, ukapita pembeni basi ni suala la muda tu, yatakauka na kupotea, ila kama kila siku unayakanyaga hayatakauka na yatakuchafua.
Mwanaume hataacha kuwasiliana naye si kwakua anampenda bali ni kwakua wanaume hawapendi tu kupangiwa. Tena kuna wakati anakua kamchoka lakini kwakua hataki kuonekana KIAZI kwa mke wake basi anawasiliana makusudi tu, ila ukimpuuza huyo mtu, ukamuona kama tope utamkwepa na atakauka maishani kwenu!
NB: Najua kuna watu badala ya kujifunza watasema “Mbona yeye ananipangia maisha kwanini mimi simpangii huu ni mfumo Dume!” Mimi nawaambia endeleeni kushindana na matope yakiwashinda njooni mnunue Kitabu changu, nipate hela wanangu waishi vizuri halafu niwape ushauri huuhuu ambao hapa nimeutoa bure!