X-WANGU ANAVYOITESA NDOA YANGU,SASA ANATAKA NIZAE NAE SIJUI NIFANYAJE! MSAADA TAFADHALI

0


Mimi ni Mama wa mtoto mmoja, nimezaa na Kaka mmoja ambaye sasa hivi ni mume wa mtu. Wakati nikiwa na ujauzito alinitelekeza na mpaka leo hajawahi kuhudumia mtoto wala kujua kuwa mtoto anaendeleaje, kusema kweli nimekubaliana na hilo na namlea mwanangu mimi mwenyewe.

Kaka nina miaka 33 sasa, nipo kwenye mahusiano na Kaka mmoja, hayapo siriasi kwani bado nasita kuwa naye kwakua sijajua kama atamkubali mtoto wangu au la. Tumekaa naye kwenye mahusiano kwa miaka miwili anakuja kwangu lakini hajui kama nina mtoto. Alimuona mwanangu na hajawahi kuniuliza kitu chochote.

Ninaishi na dada yangu hivyo anaamini ni mtoto wa dada yangu kwani wanapendana sana. Sababu ya kuja kwako Kaka ni hivi, kuna kipindi nilimtafuta X wangu, nilikua tayari kubebe mimba nyingine, kiukweli sitaki wanangu kuwa na Baba toafauti na ndiyo kitu kinanizuia kuwa siriasi na huyu mwanaume niliyenaye. Baada ya kuongea na X wangu nilimuambia kuwa nataka kubeba mimba yake ili wanangu kuwa na Baba mmoja lakini alikataa kakata kwani kipindi hicho yeye ndoa yake ilikua changa.

Ana mtoto mmoja ambaye amezaa na mke wake, sasa juzi kanitafuta na kuniambia kuwa, mke wake amegundulika kuwa ana uvimbe kwenye kizazi hivyo amefanyiwaupasuaji na hawezi kutapa mtoto tena. Aliniomba kama inawezekana nibebe mimba yake na kuniahidi safari hii atahudumia, kaniomba msamaha sana na kidogo kashaanza kutuma matumizi ya mtoto.

Niko njiapanda Kaka, nataamnai kuzaa naye ili wanangu wasiwe na Baba tofauti lakini nahofia huyu mwanaume niliyenaye je atanielewa. Nahisi kama ataniacha,  kuna wakati nawaza hata kubeba mimba ya X wangu nimsingizie huyu mwanaume ili wanangu tu kuwa na damu moja lakini najua X wangu atataka mtoto, nachanganyikiwa kwakweli, sijui nifanyeje, je ni wkeli X wangu atanisaidia kuhudumia? Nisaidie kaka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top