Aliniacha na kwenda kuvalishwa PETE na mwanaume mwingine sasa anadai turudiane tena! Sijui nimrudie au nikatae

0

Mimi ni kijana wa miaka 33, sijaoa lakini nina mchumba nampenda sana. Sababu ya kuja kwako nikuwa, nimekua kwenye mahusiano na mchumba wangu kwa miaka sita sasa. Mimi nafanya kazi mwanza na yeye anaishi dar, kwakua tuliamua maisha yetu yawe dar basi tulinunua kiwanja, tukaanza ujenzi na mimi nilikua natuma pesa yeye kwakua yupo kule basi anasimamia.


Tumejenga, tumefungua Biashara na kila kitu anasimamia yeye. Tatizo nikuwa, tangu mwaka jana nimekua nikitaka kwenda kwao kujitambulisha ananipiga kalenda, mara mdogo wake anaolewa, mara huko kwao kuna sherehe mara hiki mara kile. Nilivumilia mpaka nikachoka, sasa mwezi wa sita niliamua kuchukua likizo kilazima ili kufanikisha haya mambo, lakini huwezi amini mpaka likizo inaisha alinikwepa kunipeleka kwao.


  • Nilirudi mwanza bila kufanikisha chochote, sasa sababu ya kuja kwako nikuwa, juzi nimeingia Instagram naona mchumba wangu anavalishwa pete na mwanaume mwingine. Kuna sherehe kubwa sana kwao, niliumia sana, nilimtafuta kwenye simu yake alikua hapatikani, niliona hapana, niliamua kwenda mpaka kwao, nilifika sherehe ishaisha.


Sikutaka kupaniki, baada ya kufika nilienda kuonana na wazazi wake na kuwaambia kuwa mimi nilikua mchumba wake. Baba yake alishangaa kusikia stori yangu lakini mama yake alisema kuwa ananijua lakini  mwanae aliamua kuolewa kwakua mimi nilikua namzungusha sitaki kuja kujitambulisha. Niliumia sana nikaona kuwa sina namna, niliamua kumtafuta mchumba wangu na kumuuliza kwanini ameamua kuniacha akasema mimi si mtu wa hashi yake, nina mapenzi ya kishamba.


Nilimuuliza kuhusiana na nyumba tuliyokua tunajenga akaniambia aliiuza, kweli nilifuatilia na kukuta ile sehemu iliuzwa lakini sijui pesa amepeleka wapi? naomba ushauri wako, mimi kwangu pesa si kitu kwani nampenda sana lakini tatizo nikuwa hataki kunisikiliza, najua amekosea na nipo tayari hata kumrudishia mahari yake huyo mwanaume mwingine lakini yeye hataki, nimehangaika lakini hataki hata kupokea simu zangu, kazi haziendi naomba ushauri wako ndugu.


JIBU LANGU; Kubali kuwa yameisha na endelea na maisha yako, huyo mwanamke kakusaliti kwakua ulikua unamuonyesha upendo wa kupitliza, ukamuamini sana mpaka akajisahau. Ukiangalia, simjui huyo mwanaume lakini kama aliuza nyumba yako nina uhakika kapeleka kwa mwanaume, ndiyo wanawake wengi wanavyofanya, mara nyingi mwanamke ukimpenda san akiasi anaweza kukufanyia chochote basi hujisahau na kudhani kila mwanaume ni kama wewe.


Akidanganywa na mpuuzi falni basi hukusahau, fanya hivi, muambie ushamsaheme endelea na maisha yako, aha kulalamika kwa mtu, acha kuhangaika kumtafuta na kama ukikwama nipigie mimi teana. Kitakachotokea ni hivi, kama ni yeye alikua anamhonga huyo mwanaume ni suala la muda tu watagombana kwakua huyo mwanamke wako alsihazoea kuhongwa.


Namna ulivyokua unamdekeza anaamini wanaume wote wako hivyo, lakini si kweli. Sasa ukishamuacha atakosa wmanaume wa kumhonga, wakumsumbua, ataanza yeye kumsubua huyo jamaa yake, na kama  jamaa ni kauzu hawatakaa hata mwaka, narudia hata ndoa inaweza isitokeee, atakutafuta, sasa kwakua wewe ni mdhaifu kwake akikutafuta anaamini kuwa utamsamahe ila akikutafuta nitafute mimi.


Narudia, huyo mwanamke kama mwanaume wake ni kauzu watazinguana na ukweli nikuwa, mwanamke akishadekezwa hivyo kupata wmanaume kama wewe ni ngumu, mimi mwenyewe sikufikii hata nusu. Akifika huko atataka kuleta nyokonyoko kama alivyokua anakufanyia atatimulie, basi usimsamehe nitafute nitakuambia chakufanya.


MREJESHO; Sijui kama umchawi au nini, lakini ulichokisema kimetokea, nilikutafuta mwaka jana kuhusu mwahamke wangu ambaye alienda kutolewa mahari na mwanaume mwingine. Aisee nilichunguza kumbe hata nyumba tuliyokua tunajenga aliuza ili  ampe pesa mwanaume kwenda kujitambulisha kwao na kumvalisha pete.


Baada ya kuachana mambo yalimuwia magumu, anafanya kazi lakini mimi ndiyo nilikua namhudumia kwa kila kitu basi ndiyo mwanaume naye kumbea alikua na mwanamke wake, yaani walikua wanagombania mwanaume wote wanamhonga. Baada ya kuona hana pesa kamuacha, mwanaume amehamia kwa huyo mwanamke mwingine na sasa hivi ana mimba.


Kama ulivyosema kuwa atanitafuta kweli amenitafuta, anaomba msamaha ananiambia katambua thamani yangu hivyo nimpe nafasi nyingine. Kusema kweli bado nampenda, sipo wkenye mahusiano kwani ni kama niliapa sitapenda tena, nilikua nimrudie lakini uliniambia nije kwako kuomba ushauri tena, naomba nisaidie nifanye nini, hivi ni kweli hatabadilika tena na kuniacha, nashindwa kuamua ingawa ndugu zangu hawataki kwakua aliniumiza sana nilikua kama chizi ila bado nampenda!


MWISHO

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top