Na Serengeti Media Centre.
Mnanka Daudi (30) Bodaboda mkazi wa mtaa wa Bomani mjini Mugumu,amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kosa la kubaka mwanafunzi.
Hakimu Mkazi wa Wilaya Judith Semkiwa akisoma hukumu katika kesi jinai namba 49/2021, amesema kulingana na kosa aliloshitakiwa nalo na kukiri kutenda kosa hilo mahakama inamhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani na milango ya rufaa iko wazi.
Awali Wakili wa Serikali Donasiani Chuwa ameiambia Mahakama kuwa mshitakiwa ambaye ni bodaboda alitenda kosa hilo Julai 9 saa 12 asubuhi mwaka huu katika eneo la Burunga baada ya kumlaghai kwa kumsaidia lifti ya pikipiki kwenda shule ya Serengeti sekondari.
Ameomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshitakiwa iwe fundisho kwa watu wengine kwa kuwa kabla ya kumfanyia ukatili huo alimtishia kwa kisu,hata hivyo mshitakiwa ameishangaza mahakama baada ya kukiri kutenda kosa na kudai alipitiwa na shetani.
Tazama video hapa chini.