KIJANA ARUSHA AJITEKA NA KUJIUMIZA ILI APATE MILIONI TATU ALIPE MADENI

0
Jeshi la Polisi Arusha linamshikilia kijana aliyefahamika kwa jina la Dickson Mungulu kwa tuhuma za kujiteka nakujiumiza sehemu ya shingo na mguu ili aweze kutumiwa shilingi Million tatu na Wazazi wake pamoja na Ndugu zake.

RPC wa Arusha Justine Masejo amesema baada yakumhoji Mtuhumiwa alisema alikuwa anafanya hivyo ili aweze kupata kiasi hicho cha fedha kiweze kumsaidia kwenye madeni yake.

"Mnamo July 25, 2021 Jeshi la Polisi mkoani Arusha lilipokea taarifa kwa mtu mmoja ambae jina lake tunalihifadhi  kuwa ndugu yake aitwae Dickson Mungulu umri (26) ametekwa ambapo taarifa hizo walizipata kupitia ujumbe mfupi wa  simu kutoka kwenye simu ya muhanga na ili aachiwe zinahitaji shilingi Milioni 3 vinginevyo atauwawa'- Jeshi la Polisi

"Baada ya kupokea taarifa hizo Jeshi la Polisi lilifanya uchunguzi wa kina na tarehe 28 July, 2021 majira ya jioni tulifanikiwa kumpata kijana aliesadikika ametekwa huko Morombo Mkoani Arusha katika nyumba ya kulala Wageni"- Jeshi la Polisi

"Baada ya kumuhoji mtuhumiwa huyo ambae mwaka 2020 alimaliza shahada ya Elimu katika chuo fulani kilichopo Arusha alibainika kuwa alitoa taarifa za uongo kwa ndugu zangu ili aweze kupata fedha zitakazomsaidia kulipa madeni yanayomkabili sambamba na hilo baada ya kuchunguza kwakina mwili wake ulibainika kuwepo na majiraha sehemu za Shingo na Miguu ambapo alikiri kujichoma mwenyewe kwania ya kuaminisha wazazi wake"- Jeshi la Polisi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
Post a Comment (0)

JIUNGE NA IDAWA MEDIA SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Telegram na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka IDAWA TV Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube & Jiunge WhatsApp 

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top